Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Kuna wimbo mmoja niliusikia zamani sana. Unaelezea mtu asipokuwa hata na tunda moja atawezaje kusimama mbele za Bwana. Anajifananisha yule mtu pale msalabani aliyeingia mbinguni bila kuhubiri injili. Nauomba huo wimbo
 
Mkuu nilisoma shule ya msingi Babati kukiwa na kina mwalimu Lawi, Ufoo,Mashausi Kitundu,Isaka na wengineo kibao...tufatane PM mkuu...nilikuwa nakaa mitaa ya kanisani Lutheran na tulikuwa tunaimba na kujifunza kupiga vyombo na watoto wa mchungaji Mjema

Kama ulifundishwa na Geofrey Mashausi alifundisha pia na Ihanja Technical lkn alishafariki (RIP)
 
Wakuu heshima kwenu, Tumepotea sana hapa wakuu, naombeni mwenye wimbo uitwao:-

KAMA NINGEFAHAMU SIKU, ULIIMBWA NA MUUNGANO SDA CHOIR MIAKA YA NYUMA HUKO.
 
Ubarikowe uliyeanzisha Uzi huu,Mimi natafuta wimbo wa RC nakumbuka baadhi ya maneno ila sijui umetungwa na kuimbwa na kwaya gani maneno hayo ni "MOYONI MWANGU! MOYONI MWANGU!,NISIPOSEMA NENO ASANTE,ULIMI WANGU UGANDAMANE". Kwa anayeujua naomba msaada
 
Back
Top Bottom