Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Daaaah nilikuwa nazitafta mno mno hizi nyimbo nami nimegoogle nikaletwa hapa nimefurah mno kupata baadhi ya nyimbo hizo
 
Mtu mwenye nyimbo za kwa Mungu hakuna mzee Shinyanga baadaye iliitwa kambarage na hitaji nyimbo kabla ya kubadilishwa. na pia kuna nyimbo kama Daniel aliona maandishi yaliyoandikwa ukutani, yaliyoandikwa wapi maandishi menemene tekeli na Peresi ufalme wenu umekwisha, kweli Daniel aposikia aliingia chumbani alipiga magoti mpaka mara tatu, linda imani yako baba.... Mwingine kwenye kanda hii ni usiwe kama tajiri, tajiri alikuwa oh maskini Lazaro hizi nyimbo ziliimbwa na kwaya mojawapo kutoka Shinyanga na kama siyo shinyanga basi inaweza ikawa Mwanza
 
Hivi wako wapi hawa waimba kwaya mfano waimbaji WA kwaya ya victoria singers, Kuna yule mdada aliyekuwa anaimbisha nakumbuka enzi hizo bado nilikuwa mdogo ila sauti yake mpaka leo naikumbuka,nyimbo kama ;mchaka mchaka mkimbilie yesu,twashangaa twaogopa,wakati WA leo,watumishi wake Mungu,tutapataje kupona na sikilizeni imani ya wengine.
 
Natafuta nyimbo ambazo zilikuwa kwenye kanda ya zamani title ilikuwa "Ulimi ni Sumu".
Baadhi ya nyimbo zilizokwemo kwenye tape hiyo ni.
1. Ulimi ni sumu
2. Yonah
3. Msifadhaike mioyoni
4. Kaini na Abel
NK..
natafuta audio hizo hata kama utaibadirisha tape kuwa dijito ntashukuru sana.
 
Natafuta wimbo huu 'nenda fanya kazi ile ya bwana, usiuhesabu muda' najua umeimbwa na kkkt ila sina uhakika ni kimara au kijitonyama. Naomba msaada mwenye nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom