Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Kuna nyimbo ya injili naitafuta..ya kiswahili..sijui nani ameimba..lyrics zake kwenye chorus ni "jehova nissi,jehova shalom..elio baba nakuabudu..jehova makaresh..jehova shama elishadai nakuinulia mikono juu"

Nisaidiane niupate wakuu.
 
Kuna nyimbo ina maneno haya

Luka 7:31-50 BHN​

Yesu akaendelea kusema, “Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: ‘Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!’ Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: ‘Amepagawa na pepo!’ Naye Mwana wa Mtu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mkasema: ‘Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watozaushuru na wenye dhambi!’

Imeimbwa miaka ya 1970s na Kwaya ya UVUKE Dodoma, anayeweza kuipata please atuwekee
 
Kuna wimbo waliimba KINONDONI REVIVAL CHOIR kiitikio "wanaimba talila talila ta,u talilata"halafu wanaendelea"nimesikia Simba akiunguruma"
Msaada please,Kama Kuna mtu anao atupie humu
 
Kuna wimbo umeimbwa na kwaya ya uinjilisti Arusha mjini unaitwa eloi lamasabatani nauhitaji kama kuna mwenye nao tafadhali
 
Kuna wimbo umeimbwa na kwaya ya uinjilisti Arusha mjini unaitwa eloi lamasabatani nauhitaji kama kuna mwenye nao tafadhali
Em ongezea maneno kidogo kama unaweza. Sijui ni huu

Alipokuwa msalabani, alifadhaika sana
Akasema Eloi Eloi lamasabakitani
Yaani Mungu wangu Mungu wangu mbona
 
Aah hivi enzi hizo si ulikuwa hujazaliwa?
Weeeh![emoji23][emoji23]
Ndo zilikuwa ngoma zetu hizo

"Yesu ameinuliwa msalabani
Kina amtazamaye ataokoka
Wokovu umetolewa kwa watu wote
Kila anayeamini atapokea
Na Roho Mtakatifu ametolewa
Kila anayeamini atapokea"

Ooh mwambie Yesu[emoji91]
 
Kuna nyimbo ya injili naitafuta..ya kiswahili..sijui nani ameimba..lyrics zake kwenye chorus ni "jehova nissi,jehova shalom..elio baba nakuabudu..jehova makaresh..jehova shama elishadai nakuinulia mikono juu"

Nisaidiane niupate wakuu.
Kaimba nack waimatha kitu kama hicho walikuwa wanapiga sana praise power radio unaanza hivi
Baba wa mbinguni unaweza wewe ulie mkuu na mwemaaaa
 
Wakuu,
Ninawiwa Kuhuanzisha Uzi Huu Ili Kuwaleta Karibu Wapenzi wa Nyimbo Za Injili za Zamani!
From the 80s,90s and the Early 2000s!
Kuanzia Barabara 13,Aict Shinyanga,Kijitonyama Upendo Group,Na N.k!
Naoma Tubadlshane Audios,Videos na Picha Waimbaji wa Zamani!
Old is Gold!
Tuonane Paradiso... Ni wimbo nausikiliza kila nikimkumbuka Mzee wangu maana ulipigwa sana kwenye msiba
 
Back
Top Bottom