Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Ukiisoma zaburi hiyo na kuishika itakusaidia sana maana Bwana anapenda tunavyopeleka mahitaji yetu na haja zetu tuwe ni wasafi wa kiroho
 
Mungu ametupa kibali tena siku ya Leo kukutana mahali hapa
Tunahitaji kupeleka haja zetu kwake yeye ni Mungu mwenye rehema nyingi

Siku ya Leo tunakutana kwaajili ya kuomba mahitaji ya kibinafsi kila mtu ataomba jambo ambalo anataka Mungu amtendee
 

Zaburi 51:1-19​

Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanifundisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
Ameen
 
Ee Bwana Mungu

Nao mkono Wako wenye nguvu uwe karibu nami na chini yangu, Ukinibeba ninapokuwa dhaifu, Ukinilinda ninaposhambuliwa, Ukinisaidia kuinuka ninapoanguka, Ukinishika karibu na moyo Wako. Ninaomba haya yote kwa unyenyekevu kwa ajili ya utukufu wa jina lako kuu-Yesu. Amina.

Zaburi 23:1,4
BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.

Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
 
IMG-20241106-WA0099.jpg
 
Mungu ametupa kibali tena siku ya Leo kukutana mahali hapa
Tunahitaji kupeleka haja zetu kwake yeye ni Mungu mwenye rehema nyingi

Siku ya Leo tunakutana kwaajili ya kuomba mahitaji ya kibinafsi kila mtu ataomba jambo ambalo anataka Mungu amtendee
Bwana Yesu asifiwe

Ni siku nyingine tena Mungu ametupa kibali kukutana jukwaa hili Leo tena tunaendelea na maombi ya kibinafsi tumpelekee haja zetu kwake yeye ni muaminifu anajibu kila ombi
Mungu sio sawa na mwanadamu yeye ni muaminifu
karibuni wote msipite kimya kimya
 
Anza kuombea eneo la kazi kabla haujaombea kazi

Siku ya Leo nimekuletea mafunuo haya ambayo Mungu amenipa
Watu wengi wamejikuta wanaombea kazi na kusahau kuombea eneo la kazi
Bila kujua Kuna umuhimu mkubwa wa kujipatanisha kazi yako na damu ya Yesu katika eneo ambalo unafanyia kazi

Neno la Mungu linafundisha jambo hili kutoka katika kitabu cha Waebrania 11

Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Basi watu wengi wanaoanzisha mradi Fulani au kupata kazi sehemu huwa wanaombea zaidi kazi/biashara wapate mafanikio makubwa
Kuombea kazi ni jambo pia zuri Mungu atakubariki

Mungu akikufungua zaidi akili yako utagundua Kuna umuhimu wakuanza kuombea chanzo Cha hayo mafanikio unayoyataka Mungu atakubariki zaidi

Kuombea eneo la kazi ni sawa na kuombea chanzo
Kuombea kazi ni sawa kuombea matokeo

Anza kuombea chanzo jipatanishe kwa damu ya Yesu katika biashara au kazi yako eneo ambalo unatarajia likupe matokeo makubwa Yale unayoyawaza kuyapata una hakika yatawezekana kuonekana

Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Kuna faida kubwa na kuanza kuombea eneo unalofanyia kazi unaweza ukatoa na sadaka kumshukuru Mungu kwaajili ya eneo hilo


Faida za kuanza kuombea eneo la kazi
Biashara yako itakua na utajenga nyumba
Kazini cheo kitapanda na utajenga nyumba
 
Leo unaposali, omba kila unachogusa kwa mikono yako kibarikiwe na kizae matunda. Kila akili yako inapotumika kufanya jambo lenye manufaa basi na likafanikiwe. Wale tunaopata riziki kupitia wao Mungu aendelee kuwabariki. Na pale vinywa vyetu vinapofunguka basi viongee busara
 
Bwana Yesu asifiwe
Tutembee na Neno katika maombi jukwaa hili bila kutembea na neno unakuwa umefanya kazi nusu
 
Bwana Yesu asifiwe
Mungu ametupa Kibali siku nyingine tena tuamke tumshukuru kwa Sababu ametuamsha salama
Haijalishi unapitia nyakati Ngumu Kiwango chako cha kumtafuta Mungu kisipungue Yéyé ananjia nyingi za kumvusha mwanadamu Katika magumu unayoyapitia
 
Asante, Bwana, kwa baraka ulizonipa juu ya maisha yangu . Umenipa zaidi kuliko nilivyofikiria. Umenizunguka na watu ambao wananiangalia kila wakati. Umenipa familia na marafiki wanaonibariki kila siku kwa maneno na matendo mema.

Yeremia 32:17
Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza
 
1Thesalonike 5:1-8
1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.

2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.

4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.

5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.

8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. "
 
Back
Top Bottom