Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 1,012
- 2,317
Ubarikiwe sana mkuu, achana nae huyo tumuombee abadirikeAhsante japo niliomba tutumie LUGHA za staa na Kwa wale ambao hawaamini katika maombi ingekuwa busara kupita tuu ili angalau Uzi huu ungewapa nafasi wale wanao amini katika maombi
AminaUbarikiwe sana mkuu, achana nae huyo tumuombee abadirike
Asisaahu na ya kutoleaMwambie atume nauli😃
Ndugu ubarikiweUbarikiwe sana kwakutuletea Uzi huu Mungu anatukumbusha tumtafute kwa bidii zote wakati wote na katika maombi ya asubuhi ni vyema tukaomba sana kwa ajili ya watu wote wakapate kukombolewa
1 Timotheo 2:1
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote
Kwa wewe unayeamka kwaajili ya kufanya maombi fanya maombi haya yenye nguvu sana na yenye kujibiwa kwa haraka
Anza kwanza kumshukuru Bwana Yesu kwa ajili ya matendo makuu aliyokufanyia wewe pamoja na familia yako siku iliyopita
malaika huko mbinguni wapo attention kusikia vilio vya watu wengi ungana nao lia pamoja na wanaolia utabarikiwa sana
Omba kwaajili ya watu wote wanaopitia mapito magumu ili wapate kukombolewa
Kuna watu wamelala na njaa ila wewe umekula umeshiba waombee
Kipindi hichi vijana wengi wanapitia hali ya kukosa ajira wanamlilia Mungu ungana nao kuwaombea
Kuna watu ulisoma nao tangu shule ya msingi hata secondary lakini hujui wanapitia mapito gani ungana nao kuwaombea wakombolewe
Mwisho ndio peleka hitaji lako kwa Bwana Yesu akutendee
Ninaomba tujulishane kwa wale walioona katika jicho la rohoni mambo ambayo Mungu anatukumbusha tuombe
Anza utaratibu wa kufanya maombi asubuhi alfajiri utajibiwa haraka sana
Bwana wetu Yesu anasema yeye ndiye mzabibu wa kweli na baba yake ndiye mkulima na sisi ni matawi pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya neno lolote. Yohana 15 Kwako wewe Kama ambaye unakutana changamoto za kiuchumi na magonjwa nk anza sasa kumtafuta Bwana Yesu katika mida hii ya kuanzia mida hii...www.jamiiforums.com
AminaNdugu ubarikiwe
AminBismillah ladhi la yadhuru maa ismih sheiun fil ardhi wa lafi samai wahuwa samiu laadhim
amenBaba katika jina la Yesu ni wewe ndiye ujazaye mioyo yetu furaha ,amani , upendo, na kutupa sisi afya na uzima , achilia nguvu ya roho wako kwa anayesoma ujumbe huu ukamfundishe kuvunja vifungo vya magonjwa ambavyo watu wako wamefungwa na mfalme wa giza yaani shetani na malaika zake ( wachawi na waganga , mapepo na majini ) katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth , fungua moyo wa msomaji wa ujumbe huu apate kuelewa ujumbe huu na apate maarifa ya kushindana na kushinda kwelikweli kupitia jina la Yesu .Amen
Amen
Ndugu watanzania kupitia Uzi huu nitakuwa Kila siku Alfajiri ninatuma mstari maalumu wa maombi Kwa wale waombaji wa asubuhi. Ufunguapo Uzi huu kuanzia saa nane kamili usiku utakutana na maneno yatakayokuongoza na kuchochea nguvu ya maombi.
MSTARI WA KUSIMAMIA
Zaburi 90:14 " Utushibishe Asubuhi kwa fadhila zako. Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote"
LUGHA;
Tunaomba Uzi huu uchangiwe Kwa Lugha nzuri yenye staha ili kuwasaidia wapenzi wa maombi ya Asubuhi kupata sehemu ya kutumiana jumbe na kuombeana. Haitakuwa busara kama hauamini katika maombi ukatukana au kukashifu jambo linaloweza kusababisha Uzi kufungwa.
Mbarikiwe na karibuni kwenye Uzi huu maalumu kwaajili ya maombi ya Asubuhi.
Asubuhi ya Leo 10/10/2024 post #13 au bofya hapo chini kupata mstari wa leo
Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Ndugu watanzania kupitia Uzi huu nitakuwa Kila siku Alfajiri ninatuma mstari maalumu wa maombi Kwa wale waombaji wa asubuhi. Ufunguapo Uzi huu kuanzia saa nane kamili usiku utakutana na maneno yatakayokuongoza na kuchochea nguvu ya maombi. MSTARI WA KUSIMAMIA Zaburi 90:14 "...www.jamiiforums.com