Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Bismillah ladhi la yadhuru maa ismih sheiun fil ardhi wa lafi samai wahuwa samiu laadhim

Maana yake
"Najikinga kwa jina la mwenyezi Mungu halitanidhuru baya lolote katika ardhi wala mbingu, Hakika wewe mwenyezi Mungu ni msikivu na ni mjuzi wa yote"

Dua ya asubuhi na jion.
 
Kuna Aya katika Quran inanibariki sana ila nimeisahau inazungumzia maneno kama " kama mwanga wa asubuhi..." Inamaneno ya faraja sana
 
11/10/2024

Amkeni katika maombi,
Mstari wa kusimamia, Matendo ya mitume 17:30
" Basi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni. Bali Sasa anawaagiza watu wote wa Kila mahali watubu"
Ndugu. Tuamke katika maombi, Leo Tunaagizwa na Mungu kuomba kwa habari ya Toba ili tuweze kuwa na msimu mpya wa maisha matakatifu Kwa Mungu. Matendo yetu ya zamani hayatahesabiwa kitu! Kwakuwa "tunaagizwa" Tutii Kwa kuamka na tuweze kufanya maombi haya maalumu ya Leo ya Kutubu. Barikiwa tuendelee na Maombi watoto wa Mungu.
images (12).jpeg
 
Ubarikiwe sana kwakutuletea Uzi huu Mungu anatukumbusha tumtafute kwa bidii zote wakati wote na katika maombi ya asubuhi ni vyema tukaomba sana kwa ajili ya watu wote wakapate kukombolewa

1 Timotheo 2:1
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote

Kwa wewe unayeamka kwaajili ya kufanya maombi fanya maombi haya yenye nguvu sana na yenye kujibiwa kwa haraka
Anza kwanza kumshukuru Bwana Yesu kwa ajili ya matendo makuu aliyokufanyia wewe pamoja na familia yako siku iliyopita
malaika huko mbinguni wapo attention kusikia vilio vya watu wengi ungana nao lia pamoja na wanaolia utabarikiwa sana
Omba kwaajili ya watu wote wanaopitia mapito magumu ili wapate kukombolewa
Kuna watu wamelala na njaa ila wewe umekula umeshiba waombee
Kipindi hichi vijana wengi wanapitia hali ya kukosa ajira wanamlilia Mungu ungana nao kuwaombea
Kuna watu ulisoma nao tangu shule ya msingi hata secondary lakini hujui wanapitia mapito gani ungana nao kuwaombea wakombolewe

Mwisho ndio peleka hitaji lako kwa Bwana Yesu akutendee

Ninaomba tujulishane kwa wale walioona katika jicho la rohoni mambo ambayo Mungu anatukumbusha tuombe

Mungu aliyemwema akuamshe katika maombi ya leo
 
Ayubu 38:12-13
[12] Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

[13] Yapate kuishika miisho ya nchi,
Waovu wakung’utwe wakawe mbali nayo?

Job 38:12-13 NKJV
[12]“Have you commanded the morning since your days began, And caused the dawn to know its place,

[13]That it might take hold of the ends of the earth, And the wicked be shaken out of it?
 
Amina mpendwa tuendelee na maombi
 
Mungu mwema na mwenye rehema, asante kwe kutupa siku hii tena kama zawadi kwa upendo wako, ulinzi wako ukakae nasi tuweze kuimaliza siku hii salama maana kila sekunde iliyopo mbele yetu ni fumbo tunaamini katika upendo wako kwa maana tumeyaona matendo yako makuu, katika jina la yesu amina
 
Back
Top Bottom