Uzi maalumu: Tabia zinazokera katika jamii

Uzi maalumu: Tabia zinazokera katika jamii

Wakurugenzi hili nalo mkalitazame!




Huu msemo wa Magufuli huwa unanifurahisha ila nakereka sana pale mtu anapoutumia kwenye mada serious kama hii ya lenadi mambombotela wa keibisii
 
Kweli kabisa mkuu. Na unakuta mwingine anaongea upuuzi tu na kuwa kero kwa wengine. Ustaarabu wa kijamii na jambo la muhimu sana.
Basi mkisafiri bus za mwanza na shinyanga na simiyu na geita huko mtakoma. Unapanda bus kuna wasukuma karibia wote, saba hivi wamefungulia redio kwa sauti wanasikiliza vitu tofauti tofauti. Na bus lina redio inaongea. Mwingine kafungulia tekno lake la betri kubwa na spika ya kelele anasikiliza nyimbo za kisukuma, mwingine mpira, mwingine diamond platnumz, mwingine vanny boy. Yani ile mijamaa inakera aisee. Na haikubali kuzima. Wageni mnateseka wenyeji hawana shida hata kidogo.
 
1. Kuna ile tabia ya watu kutema mate dirishani gari ikiwa inatembea huwa yanarudia dirishani la nyuma, usipokaa kitaalam yote yako.
2. Tabia za kukojoa kwenye machupa na kuyatupa hovyo.
3. Kutupa mapedi na kondomu maeneo ambapo watoto Ni rahisi kukutana navyo.
4. Kufungulia redio Kama una semina chumbani kwako haijalishi ni muda gani iwe night au mchana ni mwendo wa Max Vol.
 
Na wengine hadi wanataja cheo chako na kuanza kukutangaza kwa watu wakati wewe hujawahi kuwaambia. Wanaudhi wee acha tu!! Unakuta umekaa mahali unapiga stori na jamaa zako hata hawajui unafanya kazi gani.......wengine wanahisi wewe ni mtu wa Usalama wa Tiafa........halafu anakuja mpuuzi mmoja kuropoka cheo chako hadharani 😀 😀 😀 😀 😀
Cheo cha wapi
 
Hata mimi nakerekwa sana na hii tabia na kuingiza kidole puani kila muda yani ndo siwez kabisa kuvumilia naweza kuhama nilipokaa
Kuna sehemu fulani nilienda kula chkula nikakuta mhudumu anaingiza kidole puani mara ka mara, nikashiba kabla ya kula nikaondoka zangu.
 
Hii tabia ya tumekutana njiani na kuanza kuniuliza naenda wapi inakera hata kama ni majirani siyo kuulizana ivyo Jamani.
 
Kuna hii tabia ya akina mama wenye watoto kupanda gari la abiria huku wakiona kabisa kwamba hakuna kiti cha kukaa kwa kujiaminisha kwamba wakiingia ndani wataonewa huruma wapishwe siti au wampe mtu aliyekaa ampakate mtoto. Sasa unakuta mtoto mwenyewe ni mliaji.....ukimpakata analia kumtaka mama hadi mtu unaona aibu na kunyanyuka kumpisha siti. Hii tabia inaudhi sana asikwambie mtu.
 
eeeh sasa kuna moja alikuwa anajifanya usalama mtaani kuna siku . katika harakati za kumwagia moyo nikamkuta kwenya bar moja akinengua.

tukakutana mtaani nikataka kumpaka akasema nikaushe ile yeye ndo kazj yake inampa ugari hapa mjini yeye sio hata usalama wa taifa
Hii umeitoa humu humu JF kuna mtu alishaihadithia
 
Kuna ile kwenye daladala mt anapanda na ammizigo yake labda bag, au ndoo n.k anakuomba umsaidie yaani mimi nakereka sana namwambia mpe konda akusaidie
 
Kuna ile kwenye daladala mt anapanda na ammizigo yake labda bag, au ndoo n.k anakuomba umsaidie yaani mimi nakereka sana namwambia mpe konda akusaidie
Mhh! Roho mbaya hiyo mkuu 😀 😀 😀 😀
 
Back
Top Bottom