Uzi Maalumu wa EPSON printers, Ushauri, matatizo, maelekezo, matengenezo nk

Uzi Maalumu wa EPSON printers, Ushauri, matatizo, maelekezo, matengenezo nk

Wasalaam wakuu,
Uzi huu utumike kupashana habari kuhusu epson printers, iwe ushauri, au kutatua matatizo mbalimbali ya hizi printer, basi taarifa zake zikusanyike hapa kuwasaidia watumiaji wengi na wenye kuhitaji kununua wanaweza kujifunza mambo mbalimbali kupitia huu uzi.
Karibuni wataalam na watumiaji wote tuyajenge.
EPSON L3050 (inkpad is at the end of its service life).

Nahitaji msaada wa kureset hiyo printer wakuu.
 
Mkuu hio mashine nilikuwa nayo ikaanza wenge nilipoenda kwa fundi akasema zijisha print page 2000 mpk 2500 huwa zinaanzaga kufa chakufanya ni kuchukuwa mpya tu maana kuitengeneza ni 250000 na mpya nilinunua 380,000 natarajia nunua nyingine mwezi wa 1 mwakani
Kwa wataalam na mafundi nina shida moja, kuna hii printer Epson L805 ina tatizo la horizontal banding au lugha ingine inaprint ila kuna vistari vidogo vidogo hutokea, nilifanya nozzle cleaning ila haikusaidia kitu, nikaja kuangalia encoder strip ilikua imechafuka na wino nikaja kununua mpya na kubadili ila tatizo halijaisha.
Msaada kipi cha ziada nitatue tatizo hili wakuu.
View attachment 1101559View attachment 1101562
 
Mkuu hio mashine nilikuwa nayo ikaanza wenge nilipoenda kwa fundi akasema zijisha print page 2000 mpk 2500 huwa zinaanzaga kufa chakufanya ni kuchukuwa mpya tu maana kuitengeneza ni 250000 na mpya nilinunua 380,000 natarajia nunua nyingine mwezi wa 1 mwakani
380,000/= ?!?!

Mkuu,

Unaijua EPSON L805 au unamaanisha L220?

Kwa hiyo bei huwezi pata L805 Bongo wala Nairobi,
Labda Guanzhou.
 
Mkuu hio mashine nilikuwa nayo ikaanza wenge nilipoenda kwa fundi akasema zijisha print page 2000 mpk 2500 huwa zinaanzaga kufa chakufanya ni kuchukuwa mpya tu maana kuitengeneza ni 250000 na mpya nilinunua 380,000 natarajia nunua nyingine mwezi wa 1 mwakani
Mmmh hiyo ulipata bei nzuri kiongozi, L805 mpya zinacheza 690,000 mpaka 800,000 kutegemea na eneo, yangu nilipeleka kwa fundi print head ilikua ya kubadilisha, na gharama ilikua 280,000/= niliona ujinga nikaamua kununua mpya 690,000/=
Printer kwa ujumla ni vizuri kununua mpya wabongo sio waaminifu kabisa linapokuja suala la kununua used items, hata kama inashida huwezi ambiwa.
 
Wakuu nahitaji kununua printer ya epson inayoweza kuprint, scan na copy kwa ajili ya stationery yangu ndogo...nina photocopy mashine kwa hiyo hii itakuwa ya kuprint coloured, ni model gani nzuri ambayo pia sio garama sana
 
Ukijibiwa unitag.
 
Nunua Epson L382 (400,000/=)
au
Epson L3050 (450,000/=).
 
Wakuu nahitaji kununua printer ya epson inayoweza kuprint, scan na copy kwa ajili ya stationery yangu ndogo...nina photocopy mashine kwa hiyo hii itakuwa ya kuprint coloured, ni model gani nzuri ambayo pia sio garama sana
Epson L382 mpaka picha inaprint, bei kuanzia 380k
 
Espon printer L220,inaandika check ink level,wakati wino upo.Tatizo ni nini?
 
EPSON L3050 (inkpad is at the end of its service life).

Nahitaji msaada wa kureset hiyo printer wakuu.
Usisahau kuweka external waste ink tank kama bado hujaweka.
artisan-700-octo-connected.jpg
 
Hii inawekwaje?

Kwenye printer za epson kuna pad ipo ndani ipo upande wa chini wa printer kuonekana mpaka ifunguliwe, ink inayotumika kusafisha nozzle & head huenda huko kama waste ink, inafika kipindi hujaa(huambatana na error message ya End of service life) kuna counters zinahesabu na kukadiria kulingana na idadi ya printed pages, hivyo huitaji kubadilishwa ili kutoleta madhara ya waste ink overflowing, sasa badala ya kuweka pad mpya unaweka mtungi wa nje utakaotumika kukusanya waste ink.

Namna ya kuweka inategemea na model ila procedure hufanana maana kuna outlet inayotoka kwenye pump humwaga huo wino kwenye pad, sasa hapo hufanyika tapping na kufungwa mrija utakaoenda mpaka nje ya printer na kisha kwenye chupa, hapo utakua umeondoa hitaji la waste ink pad.

Waste ink pad ni kama hii
hj.jpg

Sehemu inayofungwa ya kutolea nje
Photo0063.jpg

Angalizo:
kufanya hili zoezi ni lazima printer ifunguliwe, sio kila mtu ni mzoefu wa kufungua printer, kuepuka kuharibu printer yako ni vyema ukapeleka kwa fundi akufanyie zoezi hili.
 
Back
Top Bottom