Uzi Maalumu wa EPSON printers, Ushauri, matatizo, maelekezo, matengenezo nk

Kama unataka kusave gharama nunua Epson zipo kuanzia laki 4 kwa mpya, wino za mitungi utatumia kwa muda mrefu.

Kuna Hp pia ni nafuu zinauzwa kuanzia 120000 ila wino zake ni gharama na pia zina ujazo mdogo.
Nimenunua Epson l 800 haina hata mwez mzee Sasa kununua nyingine itakua mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo Dom maeneo gani
 
Wakuu nahitaji kununua printer ya epson inayoweza kuprint, scan na copy kwa ajili ya stationery yangu ndogo...nina photocopy mashine kwa hiyo hii itakuwa ya kuprint coloured, ni model gani nzuri ambayo pia sio garama sana
Anza na L 382 BEI YAKE PIA NI RAFIKI SANA

sent from toyota Allex
 
L382 roller zinawahi kuisha nadhani inategemea na aina ya karatasi, ila kuna L365 nilinunua used inapiga kazi nzuri kuliko L382 niliyonunua mpya.
Ukitumia plain paper kwa wingi, head inachoka. Ukitumia gloss paper sana, roller zinakufa. Hizi ni normal use machines tofauti na matoleo mengine. Hii 382 ni sawa na 220 na 210.
 
Nipatie mawasiliano yako mkuu tufanye biashara ya Epson l382 kama upo nazo
Nilizonazo ni za matumizi kiongozi, Pia ni bora ukanunua mpya, Wauzaji wa used wengi sio waaminifu, hawezi kukwambia matatizo au kama ilishapelekwa kwa fundi kwa tatizo lolote.
Kuna duka fulani lilikua kariakoo Zawadi technology jina lao ila wamehamia posta, huwa nanunua printer kwao wana bei nzuri kidogo.
Kwa huku Dom bei za mpya ni ghali sana.
Kuna L805 nilinunua mpya 690,000/= Dsm, ila huku dom kuna maduka yanauza mpaka 1.3M hiyo printer unaweza kujionea mwenyewe.
 
Sawa mkuu maana last time l382 nilipata kariako kwa 380
 
Kwa wale wenye printer za epson na inakuletea ujumbe huu "inkpad is at the end of its service life" usichanganyikiwe wala kuwaza. Lipo suluhisho kwa gharama nafuu sana na unapata huduma ndani ya dakika kumi tu kutoka kwetu.

Pia iwapo utaelekezwa na ukashindwa kutatua tatizo, tunakuunganisha nasi mojakwamoja ofisini kupitia Team Viewer (hii ni application inayounganisha mtumiaji mmoja kwenda kwa mwingine na kumpa access mmojawao kutumia pc/android devices hata kama yupo mbali)

Pia kwawale wanaohitaji Printer mpya za epson, zinapatikana aina zote. Tunatuma mikoani kwa uaminifu kabisa.

Karibu sana Evatony Solution tukuhudumie.
Mawasiliano: +255767086446(calls, sms, WhatsApp)
 
Pia ni vema ukaingua kwenye printer properties alaf select unachotaka kuprint kama ni document iwe ni standard quality na kama ni picha bas chagua quality iliyo juu itasaidia mimi ndo nafanya hivyo mara kwa mara ikitokea hivyo hasa ninapoprint passport na imesaidia
 
L382 iko na huo ujumbe
 
Wakuu, PRINTER ya EPSON L3110: Ina tatizo la kuwaka kwa ku_blink taa zote (nyekundu na kijani),

Inaprint vizuri.

Ila haitoi copy wala haiscan.
Na ina miezi mitatu tu tangu inunuliwe.

Naomba mwongozo wa utatuzi wa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…