Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Biblia ina tumaini lote...

Tumaini jema katika kitabu cha Mashimo ya Mfalme Sulemani habari za faraja walizokua wanasimuliana katika njia ya jangwa pasina tone la maji kutafuta almasi kwamba maisha ni nini basi zaidi ya mbegu iliyopandwa ichanue izae ife na kupeperushwa mbali na upepo? kila jambo limeshapangwa sisi tunapaswa kuishi kutafuta kidogo na kuridhika tukisubiri kwa furaha ukomo mbegu iliyopandwa.
 
When am down she cheers me up... mahondaw wangu...
When am sick she looks after me ... mahondaw
When am sad, she comforts me... mahondaw wangu...
When am super excited she gives me all whats sweet... mahondaw...
In good times and bad times she shoulder to shoulder with me...

I love her... Yes i love her... I love mahondaw more than anything...


Cc: mahondaw
 

Nimeshaona message zako nyingi kuhusu Mahondaw lakini nina wasiwasi kama yeye anakupenda umpendavyo, its none of my business ila mmmh umezidi banaaaa.... nyie ndio mnaojinyongaga siku mkipigwa kibuti
 
Isaya 45
2. Nitakwenda mbele yako na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma. 3. Nami nitakupa hazina za gizani na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wako.
 
Kweli kabisa mtoa post majoto maana hata maandiko yanasema chuma hunoa chuma.

Ukifikiria maandiko kwamba hayasemi maishayatakuwa mteremko, lakini Mungu anatupa ahadi madhubuti sana ambazo ni kweli ubinadamu mara nyingi unatuzidi nguvu na tunashindwa kuzizingatia. na hapo ndipo suala la kutiana moyo linapoingia.

Lakini hiki ndicho kipimo ambacho hata hatujawahi kukifikia cha ugumu na uzito ambao anatuponya nao.

Zaburi 86
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3 Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.


Mtihani mkubwa kabisa uko kwenye kuendelea kushikilia (kuamini) kwamba ananivusha, ananivusha, ananivusha.
Hapo tu.
 

Asante. Mioyo yetu inahitaji faraja ili iweze kustahimili maisha ya leo. Mambo mengi yanatuumiza lakini tunahitaji kusonga mbele kwa kusaidiana kwa upendo.
 
1Petro 5:6-7

6. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7. huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Yeeees! hatuna haja ya kuwa wanyonge.......😀
 
Unapozaliwa kitu cha uhakika kukipata ni kifo tu, vingine vyote unatafuta.
 
Wakati mwingine katika maisha usipigane nayo saaana na kuwaza kupita kiasi. Wakati mwingine ukiona kitu hakiendi usilazimishe, relax Muombe Mungu.
Zaburi 35
Eee Bwana, utete nao wanaoteta nami, upigane nao wanaopigana nami. Uishike ngao na kigao, usimame unisaidie. Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako.

4. Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu, Warudishwe nyuma, wafadhaishwe wanaonizulia mabaya. Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini.....

Muwe na siku njema wapendwa
 
Isaya 41
6. Wakasaidiana kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake uwe na moyo mkuu

Jamani tusaidianeee hata kuchangiana pesa za kusomesha watoto/ndugu zetu. Kipindi tunachoishi ni sheeeedah
Fungu la mama yangu hili dah!
 
7. Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike.

Tutiane moyoooooo
Haya mawili yamenifanya nikue kiimani maishani
Isaya 41
6. Wakasaidiana kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake uwe na moyo mkuu

Jamani tusaidianeee hata kuchangiana pesa za kusomesha watoto/ndugu zetu. Kipindi tunachoishi ni sheeeedah
 
Make peace with your past so that it doesn't spoil the present nor the future.
 
Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Tazama wote walioona hasira juu yako watataharika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.

Kwa maana mimi, Bwana Mungu wako nitakushika mokono wake wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia@.

Muianze wekend salama wapendwa BlessedHope JICHO TAI Joseverest kampelewele miminimkulimaakachekasana Mr Miller Perfectz Smart911 Translator Biobenga cyrustheruler
 
Emmanuel-God with us.Mungu ameshasema yupo pamoja na nasi.tumtumainie yyeye tusiogope kwa lolote lile duniani hapa
 
Amina nawe pia uwe na weekend yenye baraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…