Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Inabidi tuwe tunaonana ndio tutafarijiana vizuri, kufarijiana kwa miandiko ngumu
 
Pole wote mnaouguliwa, poleni wote mliofilisika komaeni ipo siku mtainuka tu,
poleni mliodanganywa kimapenzi kisha mkaachwa poleni ila mjikaze mtapata wenzi wengine walio wema kwenu,

poleni wote ambao mabosi wenu wanawanyanyapaa kazini jipeni moyo na kujipanga jinsi ya kupata mtaji wa kujiajiri,

poleni wahitimu wote ambao kwa muda mrefu hamna ajira au mmepata ajira ambayo kipato chake ni kidogo sana kiasi kwamba ukipata pa kutokea utakimbia bila kugeuka nyuma.

Poleni mliofiwa,
poleni mliotumbuliwa siku si nyingi mtapata kazi nyingine.

Poleni sana.
 
Mkuu usisite kushare nasi kuna cha kujifunza...
 
Jamani mi bado naendelea kupitia kipnd kigumu na bdo sijajua hatma yake

In short niko kipindi kigum ki uhalisia
Pole mkuu...amini utapita kwenye hicho kipindi kigumu, it's the matter of time....

NB: usiache sala
 
Hapo mwisho I wish kila mtu apasome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…