Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Inabidi tuwe tunaonana ndio tutafarijiana vizuri, kufarijiana kwa miandiko ngumu
 
Pole wote mnaouguliwa, poleni wote mliofilisika komaeni ipo siku mtainuka tu,
poleni mliodanganywa kimapenzi kisha mkaachwa poleni ila mjikaze mtapata wenzi wengine walio wema kwenu,

poleni wote ambao mabosi wenu wanawanyanyapaa kazini jipeni moyo na kujipanga jinsi ya kupata mtaji wa kujiajiri,

poleni wahitimu wote ambao kwa muda mrefu hamna ajira au mmepata ajira ambayo kipato chake ni kidogo sana kiasi kwamba ukipata pa kutokea utakimbia bila kugeuka nyuma.

Poleni mliofiwa,
poleni mliotumbuliwa siku si nyingi mtapata kazi nyingine.

Poleni sana.
 
kuna kipindi nilipataga misukosuko
nilitamani Dunia ipasuke...ilifikia kipindi nilitamani hata nigongwe na gari au kitu kibaya kinipate ili nife but haikuwa hivyo...
ni vile unapita wakati mgumu hata ndugu/rafiki na mpenz wanakukimbia ni hatari sanaaa
tangu hapo sikutaka tena kuamini/kuwategemea watu......
nilijiapiza na Mungu wangu na kuweka ahadi na Mungu wangu
from now nakula mema ya Nchi japo sijafikia but atlest now...naona mwanga mkubwa wa maisha yangu tofauti na kipindi cha Nyuma...
Kuna wakati now nadhani bado nipo ndotoni coz siamini kama ndiyo Mimi ambaye watu walinicheka na kunidhihaki....
hata walionitenga Leo ndiyo wakwanza kuninyenyekea...
nilichojifunza
wakati mwingine Mungu anaruhusu upitie magumu ili akufikishe kwenye kusuidio na sehemu aliyokuandalia...
lait kama wale niliowategemea wangefanya kama nilivyodhani au lait kama baba asingenitelekeza pengine leo "NISINGEKUWA MTU MAALUMU" katika Dunia yetu. ....

Natamani Kushare Nanyi story abt My life
Mkuu usisite kushare nasi kuna cha kujifunza...
 
Jamani mi bado naendelea kupitia kipnd kigumu na bdo sijajua hatma yake

In short niko kipindi kigum ki uhalisia
Pole mkuu...amini utapita kwenye hicho kipindi kigumu, it's the matter of time....

NB: usiache sala
 
Maisha bana pesa hakuna, mpenzi hakuna, familia hakuna, rafiki hakuna, ndugu jamaa ovyo.

Mvurugano kama roast la biriani ila ni kupambana tu.

Kuna kipindi mpaka unaweza sema umekuja kufanya nini kwenye hii dunia, mvurugano tu.

ILA

Marufuku Kukata tamaa.
Hapo mwisho I wish kila mtu apasome
 
Back
Top Bottom