Uzi maalumu wa kujua gharama za ujenzi wa majengo mbalimbali

50 mil inamaliza ila kwa kujibana. Ukijiachia hesabu 60mil
 
Bro sijawah kujenga ndo naanza kwa mara ya kwanza though nilishariki ujenzi kwa Bi mkubwa nilikua tu natuma pesa, sasa mwaka huu nataka nijenge mwenyewe ndo mana nikaomba tathimini ya gharama zake zote kwa ujumla
 
Ila nilichopewa na jamaa mwingne wa nje ya JF amesema kiwanja cha 20*20 hakitoshi pia akasema nisiope gharama nianze taratibu,

Tafuta mafundi wawili, wapeleke site Kwa nyakati tofauti, wape hiyo ramani, wasikilize Kila mmoja anakupa gharama kiasi Gani.

Pia wakuandalie gharama Kwa hatua, mfano msingi peke yake, kuinyanyua boma Hadi lenter, lenter yenyewe na zile mistari za tofali baada ya lenter.
Akuandalie upauaji ( mbao, bati), ije madirisha, maji na umeme, frame za milango, tiles, lipu na rangi.

itakusaidia kujipanga Kwa Kila hatua kulingana na uwezo wako.
 
Mkuu naona kama hiyo ni nzuri, nyumba ina nafasi ya kutosha, ila naona kama kiwanja chako ni kidogo, itaenea ila itabana sana

Kingine mkuu kwa hiyo nyumba ukipewa gharama za jumla utakata tamaa, wewe anza kuchimba msingi mdogo mdogo utamaliza.

Hongera sana kwa kuwaza ujenzi, nyumba ni kila kitu.
 
Asante kwa ushauri
 
Kama kweli unania ya kuanza ujenzi ni suala la kumpelekea fundi aingalie au mchora ramani muifanyie tathmini kama kuna sehemu za kurekebisha na suala la gharama
Hapa jf ni sawa ila utapata maoni ya jumla jumla
 
Bro sijawah kujenga ndo naanza kwa mara ya kwanza though nilishariki ujenzi kwa Bi mkubwa nilikua tu natuma pesa, sasa mwaka huu nataka nijenge mwenyewe ndo mana nikaomba tathimini ya gharama zake zote kwa ujumla

Lengo langu alikua kukutisha mkuu, nlitaka angalau nikupe picha ya uhalisia ujipange vizuri! Kwa ramani hyo japo haina dimension roughly kama unapenda upate kitu kizuri inaweza kucost 60-70 pamoja na fence! Ila kama kiwanja chako ni 20 kwa 20 nakushauri utafute ramani nyingne ili upate nafasi ndan hata ya kupark gari na land scaping! Alafu kingne hyo ramani ina kona nying sana itaongeza gharama upande wa bati, kenchi na kuta! Pia vyoo na jiko vipo mbali mbali itkufnya nje uwe na chemba nyingi za maji taka.
 
Asante mkuu
 
La nn lote hili acha ujinga

Mnyiramba amejenga kagorofa kake kama hiki nimeona mahali
Hongera[emoji847]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…