Unasajili vp bila kocha?
Bongo bhana, hata huko Ulaya Kocha akitimuliwa yule anayeletwa huwa anakuja kunusuru timu, na hatua ya kwanza ni kuwajengea wachezaji imani tu wapambane na sio mbinu zake.
Mbinu huendana na aina ya Wachezaji, mfano Kibu Denis kwa namna anavyocheza, kujiposition unaina kabisa kwa Nabi hawezi cheza kabisa, pia ukija kwa Pablo ukimchukua Kiungo kama Aucho au Chama kwa kocha kama Pablo hawezi kitoboa maana Pablo anapenda viungo wenye kuwa na speed na nguvu nk.
Hivyo Simba wangeanza na Kocha kisha kocha, aingalie Simba katika angle zote, yaan ile Simba ambayo inafungwa kizembe, na ile ambayo inapambana kwa jasho na damu, kupitia hapo kocha atajua ni wachezaji gani wanabaki katika kiwango chao, iwe wamefungwa au kushinda. Hapo ndipo maboresho ya kikosi hutokea.
Kwa usajili huu ni wazi sasa Simba inarudi ilipotoka Yanga ambapo walikuwa wanasajili kwa mihemko, msimu unaoisha huu Yanga imesajili wachezaji ambao sio tu kocha alijaribu kuwaona bali alipendekeza kutoka ukanda wetu huu huu wa Afrika Mashariki.
Simba wasisajili kama Ndondo Cup, watulie, natamani sana kuona Simba na Yanga zote zikifika hatua ya Makundi this time na ikiwezekana Nusu Fainali ya CCL. Ila mikurupuko hii naona kabisa Jwaneng wanakuja kutufumua hapa hapa tena.