Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

1655465604312.png


Imeelezwa Yanga imepanga kufanya usajili wa beki wa kushoto Mutambala raia wa DR Congo baada ya kumkosa mbadala mzuri wa kucheza eneo hilo na kulazimika kutumiwa Kibwana Shomari ambaye ni beki wa kulia.

Mutambala raia wa DR Congo, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Bravos do Maqui ya Angola, pia amewahi kucheza GD Interclube (Angola), AS Vita (DR Congo) na Mouscron ya Ubelgiji

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Kamati ya Mashindano ya Yanga, kimeliambia chanzo cha Gazeti la Spoti Xtra kwamba, Nabi ndiye aliyependekeza usajili wa beki wa kushoto wa kigeni kuelekea michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mtoa taarifa huyo “Tunafurahia sana usajili wa msimu huu, kocha Nabi amepania kusajili wachezaji wachache na kuacha wachache, ila amesema kabla ya kuachana nao, ni vema akahakikisha anapata wachezaji bora na wenye uwezo sahihi wa kumwezesha kufikia malengo yake kimataifa.

“Kutokana na hilo, tayari amepewa mchongo na Djuma na Bangala wa kumsajili beki wa kushoto kutoka Angola, ambapo pia naye amejiridhisha ubora
 
1655465702043.png


MAMBO LOADING DEAL BADO HALIJAWA MNIGERIA HUYU ANAKIPIGA PALE COAST WAKATI HUO SOPU NAYE ANAHITAJIKA NA SIMBA PIA
 
View attachment 2263662

Imeelezwa Klabu wa Simba SC imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu ya Bechem united FC ya Ghana Augustine Okrah.

Taarifa zilizopatikana leo Jumatano (juni 15) zinaeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ana nafasi kubwa ya kutua Msimbazi mwishoni mwa msimu.

Okrah atasaini mkataba na Uongozi wa Simba SC wa miaka miwili, huku kukiwa na kipengele kidogo cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, kama mambo yatamnyookea katika msimu wake wa kwanza.

Okrah ambaye ana sifa ya kucheza kwa kasi huku akiwa na ujanja ujunja mwingi wa kuihadaa safu ya ulinzi ya timu pinzani, amefunga mabao 14 katika michezo 31 kwenye Ligi Kuu ya Ghana msimu huu 2021/22.

Hadi msimu wa soka nchini Ghana unamalizika Okrah alikua miongoni mwa wachezaji waliotajwa sana, kuwa na kiwango bora na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakawana Tuzo katika Ligi ya nchi hiyo kwa msimu huu 2021/22.
Kumbe contract yake inaisha tarehe 30.06.2022
Screenshot_20220617-144025_Chrome.jpg
 
1655726655659.png


Unaambiwa

Simba SC bado hawajafkia makubaliano na Morlaye Sylla (23) ya maslahi binafsi.

Mazungumzo yanaendelea na klabu yake kwa wiki zilizopita.

Sylla anavutiwa na wababe wa Morocco, Raja Casablanca na Wydad AC.
 
20220620_182936.jpg

BAADA ya kumalizana na Moses Phiri kutoka Zanaco ya Zambia ikimpa mkataba wa kuitumikia Simba, mabosi wa timu hiyo hawajalala kwani wamenasa mashine nyingine mpya kwa ajili ya msimu ujao.

Usiku wa Jumamosi mabosi hao walipambana na kufanikiwa kunasa saini ya Habib Kyombo kutokea Mbeya Kwanza aliyojiunga nayo dirisha dogo la usajili akitokea TS Sporting ya Afrika Kusini.

Mwanaspoti lilielezwa baada ya mvutano wa muda mrefu kwenye kikao cha kukubaliana masuala ya kimaslahi Kyombo akiwa na wasimamizi wake pamoja na viongozi wa Simba mwisho wa siku walikubaliana.

Inaelezwa baada ya mvutano huo Kyombo alikubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba msimu ujao na sasa atarudi Mbeya Kwanza kumalizia tu michezo iliyobaki Ligi Kuu.

Simba imevutiwa na Kyombo kutokana na uwezo aliouonyesha kwenye ligi amecheza mechi chache ndani ya mkopo wa miezi sita, ila hadi sasa amefunga mabao matano ambayo ni muhimu na kati ya hayo kuna yaliyoipa pointi pamoja na kutoa pasi ya mwisho moja. Simba imedhamiria kuboresha kikosi ili kurudisha makali waliyoyakosa msimu huu ndio maana iliposhindwa kukubaliana kumlipa Kyombo maslahi ya miaka mitatu inaelezwa ikamsainisha miaka miwili.

Mwanaspoti linafahamu Kyombo na uongozi wake kwenye kikao hicho cha kukubaliana kilichofanyika kwa kiongozi mmoja wa juu, walikuwa na hali ya kujiamini katika maslahi kutokana na uwepo wa ofa nyingine mezani ya maana kutoka Singida Big Boys, ila mwisho wa siku mabosi wa Simba walipambana na alinyanyuka kwenye kikao akiwa amesaini miaka miwili.

ADVERTISEMENT

Ofisa mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema masuala yote ya usajili wa wachezaji wapya na wale wanaomaliza mikataba wakishakamilisha wataweka wazi kupitia mitandao yao ya kijamii.

“Tunaendelea na vikao vyetu kuhakikisha tunapata kocha mpya mzuri pamoja na kufanya usajili wa wachezaji wa maana kulingana na mahitaji ya timu yetu. Baada ya kukamilisha haya mawili tutayaweka wazi kama kawaida ya Simba ilivyo,” alisema Barbara na kuwataka mashabiki wa Simba watulie kwani wapo kwenye mapambano ya kuboresha timu ili kurudisha furaha iliyopotea msimu huu.

Naye ofisa mtendaji wa Mbeya Kwanza, Gideon Ngereza alisema akili yao kwa sasa ni kupambana kushinda michezo mitatu iliyobaki ili kumaliza msimu kwenye nafasi nzuri

“Kutokana na hali yetu ilivyo tunahitaji uwepo na uwezo wa mchezaji kama Kyombo ili kutoa mchango kuhakikisha mechi zote tunashinda, ila kutokana na ubora wake ni ngumu kubaki naye kikosini msimu ujao,” alisema Gideon.

“Mezani kwetu tunafahamu kuna timu mbili zinamhitaji ila naamini kuna moja kati ya hizo atakubaliana nayo ila mwenyewe au hiyo timu ndio wanaweza kuweka wazi.”

Kyombo alianza kufahamika katika soka hapa nchini akiwa na kikosi cha Mbao kabla ya kutimkia Singida United ambako nako hakukaa muda mrefu alienda kucheza soka kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini katika klabu ya Mamelodi Sundowns.

Mamelodi ilimtoa kwa mkopo TS Sporting ya nchini humo kabla ya kumtoa tena kwa mkopo wa miezi sita Mbeya Kwanza na mkataba wake sasa mwisho wa msimu huu unafikia mwisho hivyo Simba inaelezwa imemsajili akiwa huru.

Credit,
Mwanaspoti
 
Back
Top Bottom