Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Tafuta hizo tetesi utuwekee hapa screenshot.
Kibe Denis
IMG_20220615_190758.jpg
 
Bernard Morrison ameshasaini mkataba wa awali wa kujiunga na Yanga. Na taarifa zinaonyesha ni chaguo la Prof Nabi!

Mashabiki tusiomkubali huyu mvuta bangi sijui tutazificha wapo sura zetu msimu ujao! I wish abadili maamuzi dakika za mwisho, halafu abakie huko huko kwao.
BM bado mzuri atatusaidia sana msiomkubali mnakosea this is football na hayo hutokea sana ktk maisha ya soka
 
Striker Lazarous Kambole wa Zambia aliyekuwa anachezea Kaizer Chiefs naye ameshasinya miaka 2 Jangwani!
Dah! Yanga ya msimu ujao, itatisha sana aisee!
Huyu msimu huu 2021/2022 amechezeshwa mechi 6 tu, goli 1, assist hakuna. Ni miongoni mwa wachezaji saba huru (sio kutoka Kaizer Chiefs) walioachwa na Kaizer Chiefs waende popote wanapotaka bure
 
Nauliza kwani Dirisha La usajiri Limefunguliwa ?? Sababu Naona Simba Wamemtangaza wamemsajiri Phiri au hii inakuwaje
 
1655465439516.png


Imeelezwa Klabu wa Simba SC imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu ya Bechem united FC ya Ghana Augustine Okrah.

Taarifa zilizopatikana leo Jumatano (juni 15) zinaeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ana nafasi kubwa ya kutua Msimbazi mwishoni mwa msimu.

Okrah atasaini mkataba na Uongozi wa Simba SC wa miaka miwili, huku kukiwa na kipengele kidogo cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, kama mambo yatamnyookea katika msimu wake wa kwanza.

Okrah ambaye ana sifa ya kucheza kwa kasi huku akiwa na ujanja ujunja mwingi wa kuihadaa safu ya ulinzi ya timu pinzani, amefunga mabao 14 katika michezo 31 kwenye Ligi Kuu ya Ghana msimu huu 2021/22.

Hadi msimu wa soka nchini Ghana unamalizika Okrah alikua miongoni mwa wachezaji waliotajwa sana, kuwa na kiwango bora na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakawana Tuzo katika Ligi ya nchi hiyo kwa msimu huu 2021/22.
 
1655465543275.png


Imeelezwa.SIMBA imepanga kumununua beki wa kulia wa Kagera Sugar, Dickson Mhilu atakayekuja kuwa mbadala wa mkongwe Shomari Kapombe.

Huyo ni beki wa pili kutajwa kuja kuchukua nafasi ya Kapombe, mwingine ni David Kameta anayecheza kwa mkopo Geita Gold ambaye amepangwa kurejeshwa Simba.

Simba hivi karibuni ilitangaza kuachana na Kameta mwishoni mwa msimu huu kabla ya Azam FC na Geita kuwania saini yake.

Simba imepanga kununua mkataba wa miaka miwili alionao beki huyo pale Kagera Sugar.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi umepokea majina mawili ya wachezaji wanaocheza nafasi hiyo ya beki wa kulia ambaye ni Dickson na Kameta kati ya hao mmoja atapewa mkataba wa miaka miwili.

Aliongeza kuwa Simba itatakiwa kuvunja mkataba wa miaka miwili kwa Dickson alionao Kagera Sugar unaomalizika 2024 huku Kameta akisaini kama mchezaji huru, kwani mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

“Kama jina la Dickson likipitishwa rasmi viongozi, basi Simba tutatakiwa kutumia fedha nyingi kuuvunja mkataba wake wa miaka miwili utakaomalizika 2024 Kagera Sugar.

“Lakini kama akipitishwa Kameta, basi huyu tutamsajili kama mchezaji huru kwani mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.
 
Back
Top Bottom