Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

1656915929762.png


🚨D O N E D E A L🚨

Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior.
Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, tumemnunua kutokea timu ya Sol FC ya kwao, akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.

Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.

Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.

Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.
 
1656916056815.png

🚨 N E W C O A C H 🚨

Tunayo furaha kumtangaza, Kali Ongala, kuwa Kocha wa washambuliaji ndani ya kikosi chetu kwa mkataba wa miaka miwili.

Hii ni mara ya kwanza kwenye kikosi chetu kuwa na kocha wa washambuliaji.

Kali ambaye amewahi kuwa mchezaji wetu wa zamani na kocha msaidizi, anakuja kuboresha makali ya washambuliaji wetu, nafasi ambayo alikuwa akicheza vema kipindi cha uchezaji wake.
 
1656920639502.png


Singida Bigi Stars wadaiwa kuvunja mkatba na Habibu Kyombo

Tetesi zinaeleza kuwa kijana katia wino Msimbazi

Wacha tuone hili dili
 
1656920945064.png


Imeelezwa KLABU ya Simba, ipo kwenye wakati mzuri wa kumrudisha kikosini hapo kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji, Luís Jose Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri.

Hiyo ni baada ya Luis kuwa na wakati mgumu ndani ya Al Ahly tangu alipojiunga na timu hiyo Agosti 26, 2021 akisaini mkataba wa miaka minne akitokea Simba.

Baada ya Al Ahly kuachana na Kocha Mkuu, Pitso Mosimane na nafasi yake kuchukuliwa na Ricardo Soares, imeripotiwa kwamba Luis hana maisha tena kikosini hapo.

Kwa mujibu wa mabosi wa Al Ahly, kiungo huyo tangu ametua hapo, hajaonesha kiwango kizuri, hivyo Soares, baada ya kuangalia tathmini ya kikosi chake, amemuondoa Luis kwenye mipango yake. Kwa sasa Al Ahly inaangalia namna ya kusajili mchezaji mwingine wa nafasi yake.

Uamuzi uliochukuliwa ni kumuachia Luis aondoke kikosini hapo iwe kwa mkopo au kuuzwa moja kwa moja, kwa sasa anasubiriwa Miquissone na wawakilishi wake kujadili hilo kabla ya kufanyika uamuzi.

Wakati Luis anauzwa, uongozi wa Simba ulisema kwamba, walikubaliana na Al Ahly kwamba mchezaji huyo endapo akiondoka Al Ahly, Simba ina nafasi ya kwanza kumrudisha hapa nchini kuliko timu yoyote ya Tanzania.
 
timu nzima ya Mikia aka Makolo FC ni mbovu na inafaa itimuliwe yote kwa kukubali kupasuliwa na Feisal na kusababisha mashabiki wake kujazana mahospitalini kutibiwa majeraha ya moyo!

pia wawatimue MOooo, Barabara na Matofali
Taratibu hatutaki fujo🤔
 
View attachment 2280909

🚨ABDUL SELEMAN SOPU NI MALI YA AZAM FC

Yes, Azam FC is Back✊Huu ndio Ukubwa wa @azamfcofficial tuliokuwa tukiuota kila siku uje! Unakwenda vitani na wakubwa wa soka nchini na unaibuka mshindi kibabe kabisa

Kazi nzuri CEO @abdulkarim.amin 👏 Well Done @yusufbakhresa ! CHAMAZI kuwe mahala panapoogopesha sna Msimu ujao
Ukiondoa kipaji chake kikubwa alichojaliwa na Mwenyezi Mungu, Yanga nayo imemsaidia kwa sehemu yake kufika hapo alipo kupitia ile mechi yao ya juzi. Hivyo ni wakati wake sasa kupambana ili afikie kilele cha mafanikio yake.

Akibweteka na kulea kitambi hapo Azam, basi ajiandae tu kuwa na kiwango kama cha kaka yake Ibrahim Ajibu na Ditram Nchimbi.
 
1657191130809.png


TETESI: LUIS ANARUDI SIMBA 🔴
.
Hadi Kufikia leo jioni tayari 90% ya dili la Luis Miquissone 🇲🇿 kutoka Al Ahly 🇪🇬 kurejea Simba 🇹🇿 linaelekea kutimia.
.
💬: “Miquissone anaipenda Simba, ameomba arejee kwenye kikosi, maana amekumbuka lile ‘vaibu’ na upendo ambao alikuwa anapewa na mashabiki wake, pia familia yake inataka aishi Tanzania. Wakati wanaongea sana, sisi tutafanya kwa vitendo, nadhani muda utafika mashabiki wetu wataanza kupata raha.” Kimesema chanzo changu makini ndani ya Simba.
 
1657191215463.png


DONE DEAL

🇨🇲 | HERVE NGOMO 🔜 SIMBA SC 🔴
.
Taarifa zinaeleza kuwa Klabu za Simba na Cototon Sport zimefikia makubaliano ya dili la uhamisho wa Beki kitasa raia wa Cameroon Herve Ngomo (26).
.
Ngomo anatua Simba kuvaa viatu vya Serge Pascal Wawa.
 
1657191362274.png

Azam wanashusha vifaa kila siku. Safari hii ni zamu ya Nathael Chilambo
 
Back
Top Bottom