Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
- Thread starter
- #301
🚨D O N E D E A L🚨
Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior.
Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Kipre Junior Zunon Tiagouri Emmanuel, tumemnunua kutokea timu ya Sol FC ya kwao, akisaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.
Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1), amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017-2018.
Kiungo huyo mshambuliaji, 22, mwenye kipaji cha hali ya juu pia aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.
Ubora wake ulimfanya pia kuchezea timu za Taifa za vijana za Ivory Coast U-15 na U-17, pamoja na kikosi cha wachezaji wa ndani (CHAN) 2020.