Ndugu wanajukwaa wenzangu,ninawasalimu kwa jina la JMT! Kwa wale ambao Mungu anaendelea kuwajaalia afya njema basi ni jambo la kumshukuru Mungu,lakini pia kwa wale ambao wana matatizo mbalimbali ya kiafya si wakati wa kukata tamaa,kwani siku moja unaweza kupata uzima wako,kikubwa ni kumtumainia yeye aliye juu.
Kuna watu wengi sana wanasumbuliwa na tatizo la bawasili na hata hapa jukwaani wamekuwa wakilalamika sana juu ya adha kubwa wanayoipata kutokana na ugonjwa huu ambao unasumbua sana jinsia zote mbili.
Watu wengi wamekuwa wakiongelea sana chanzo chake na namna ulivyo,kwa hiyo sitajikita kueleza mambo yaleyale ambayo yanaandikwa kila siku.
Kwa wewe unayesumbuliwa na tatizo hili na yawezekana umepita sehemu nyingi bila mafanikio,yawezekana tiba hii ikakusaidia na ukarudi hapa kutoa ushuhuda acha kupuuza.Najua dawa ni code ya mtu kwa ajili ya kipato chake na hata kwangu pia,lakini nimeamua kufanya makusudi ili japo nisaidie wahitaji maana nawahurumia sana.
Tafuta mti unaitwa mjafari,chimba mizizi yake(Nilishawahi kuuandika hapa) kwangua maganda ya mizizi yake vizuri na uyaanike sehemu isiyokuwa na jua kali ili kutokupoteza ubora wake (mzizi wake ni mkali,ladha ya tangawizi na uchungu mkali ndani yake).Baada ya kukauka vizuri,tafuta sufuria uikaange mpaka iingue kama mkaa,baada ya hapo saga vizuri uwe unga mweusi kama wa mkaa.
Tafuta kuna nta ya miti inaitwa DEMOAI ukiingalia vizuri inafanana na asali ikiwa kwenye chupa,ni maarufu kwa jina hilo bila shaka ni kimasai maana wao ndiyo wanaiuza sana,ingawa wanaichakachua kwa kuiongezea mafuta ya kula ili iwe nyingi kwa hiyo inaathirika na kutokuwa na ubora unaotakiwa,kama unaweza kupata pure kabisa ni jambo jema.Hii inapatikana kwenye mapori ya Morogoro,Arusha na hata pwani kidogo,lita moja inaweza kuuzwa zaidi ya laki moja.
Chukua kiasi kidogo cha unga wako wa mjafari ulioundaa kama nilivyoelekeza ( nusu kijiko kwenye kiganja) changanya matone mawili ama matatu ya nta (DEMOAI) changanya vizuri ichanganyike tayari kwa kupaka sehemu yenye tatizo.
Hakikisha unapaka mara mbili kwa siku.
Kama unakuwa na tatizo la kinyesi kigumu tumia matone yasiyozidi matatu ya nta hiyo (DEMOAI) kwenye kikombe kizima cha chai ukoroge vizuri kila siku asubuhi hutajuta tena kujisaidia huku ukitibu bawasili kwa mtindo huo wa kupaka.
Kama bawasili ni za ndani,kuna mti maarufu sana sisi wasukuma tunauita NSUHA( nilishawahi kuandika miujiza yake hapa) huu ni maalum kwa kutoa vimbe za aina zote mwilini unapochanganywa na aina nyingine ya mimea.Tengeneza unga wa mizizi yake na utatumia kijiko kimoja katika maji moto mara tatu kwa siku.
Note: Tiba hii inawasaidia watu wengi na wengi wamepona kabisa.Acha kuzarau mitishamba.Ukipona kumbuka kutoa sadaka kwa Mungu wako.
Ahsante!!
Sent from my TECNO BA2 using
JamiiForums mobile app