Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Mkuu @binnun Crocodiletooth

Msaada jinsi gan naweza kuisafisha pesa iliyofungwa isizalishe...yaan iko hiv kuna ndugu yangu anafanya kazi kwa tajiri fulan sema yule tajiri kaifunga hela yake kiasi kwamba hawezi kufanyia biashara yoyote au akifanya ataishia kupata hasara na hela ikamalizika yote..hata akitafuta mtaji sehem nyingine akiweka kwenye biashara akichanganya na ile tu bas inaisha yote

N.B MSHAHARA LAZIMA WAPEWE KWENYE BAHASHA...NA HAWAPEWI SIKU YA JUMATATU
Weka bank, ikae kwa siku 7 itoe fanya yako, maana sumu ya pesa za namna hiyo ni kuikojolea tu, lakini huenda pia tatizo likawa juu yenu na biashara yenu.
 
Mkuu, Tunaomba tupe baadhi ya aina za mafuta ya mgando yanayofaa e.g. yatokanayo na wanyama e.g. samli n.k. au yale ya dukani e.g. vaseline n.k. Asante kwa ku-share.
Namanisha mafuta ya mgando ya kupaka mwilini mfano baby care,na mengineyo utakayo pata
 
Turmeric au manjano ni dawa nzuri mno kiasi haipaswa mtu kukosa ndani mwake, pia ni dawa nzuri nambari moja kwa matatizo mengi ya ini.
Asante sana mkuu kwa endorsement. Naomba kama hutojali hebu tuelezee faida zake zaidi. Na kwa Ini inasaidia nn haswa.
 
Habarini ndugu, wataalamu na mnaojifunza kama mm LCP hapa.

Kijana wangu amekua na changamoto na kuwashwa na kutokwa vipele, tulipoenda hospitalini tukiambiwa ni pumu ya ngozi. Tumepewa madawa anatumia lkn inarejea tena. Basi tukaamua tumpime allergy, napo tukakuta ana allergy kibao, baadhi ya vitu tulivyoambiwa asile kwa kweli tumeacha na ngozi yake ikaanza kutakata kiasi.

Sasa hivi karibuni naona ile hali ya kuwashwa na vipele imerejea tena. Naombeni ambao mmewahi kupitia shida ya namna hii na mkapata suluhu mnisaidie.

Naomba pia wataalam wa mimea tiba kama kuna kitu nnaweza kumuandalia, dogo anateseka sana akianza kujikuna utamuonea huruma. Ni mdogo wa mwaka mmoja.

Asanteni [emoji120]
 
Ndetere
jaribu kusema maneno kwa lugha uijuayo wewe pale utakapopata kiu ya kuvuta sigara.

Go behind me evil spirit (7 times)
Endelea kurudia tu hamu ikikujia. Ukiwa na nia thabiti utaacha kwa msaada wa MUNGU.
Asante mkuu nitafanya ivo... have a nice weekend
 
Uzi wa Kuishi nao milele,
Pongezi kwa watoa elimu na wachangiaji wa kawaida hadi kufikia hapa,
Asanteni sana,

Tiba
kipande cha mti wa muhogo ukiwa safarini hasa zile safari za miguu hakikisha unashikiria mkononi pia usithubutu kubadilisha mkono hiyo ni tiba kwa watu wabaya uwapo safarini,
Lakini kama safari yako si ya miguu basi pata kipande weka mfuko wa suluari au sketi au gauni lako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mwenye kuufahamu mti huu tafadhali...
Kuna dawa fulani ya mtu aloungua na
moto, uwe umetokana na uji,chai au vyovyote vile,
Nakumbuka bibi yangu alikuwa anabandua magome ya mti huo kisha baadhi anapata unga na magome mengine anachemsha kwa kuongeza na maji na baada ya mchemsho huwa na rangi nyekundu kama damu, maji haya ni kwa ajili ya kusafishia vidonda tu na
ule unga wa magome uliosagwa ulikuwa na rangi nyekundu au pinki fulani na hutumika kupaka sehemu zote zilizoungua na moto kisha mgonjwa anaweza kukaa kama siku tatu hivi anaangaliwa kidonda kinaendeleaje ili kufahamu kama kuna ulazima wa kuosha tena na kubandika upya dawa,
KUMBUKA
ya maji ya kusafishia uwe unapasha joto kutokana na uvumilivu wa ngozi ya mtu unaemtibia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom