...Mwenye kuufahamu mti huu tafadhali...
Kuna dawa fulani ya mtu aloungua na
moto, uwe umetokana na uji,chai au vyovyote vile,
Nakumbuka bibi yangu alikuwa anabandua magome ya mti huo kisha baadhi anapata unga na magome mengine anachemsha kwa kuongeza na maji na baada ya mchemsho huwa na rangi nyekundu kama damu, maji haya ni kwa ajili ya kusafishia vidonda tu na
ule unga wa magome uliosagwa ulikuwa na rangi nyekundu au pinki fulani na hutumika kupaka sehemu zote zilizoungua na moto kisha mgonjwa anaweza kukaa kama siku tatu hivi anaangaliwa kidonda kinaendeleaje ili kufahamu kama kuna ulazima wa kuosha tena na kubandika upya dawa,
KUMBUKA
ya maji ya kusafishia uwe unapasha joto kutokana na uvumilivu wa ngozi ya mtu unaemtibia.
Sent using
Jamii Forums mobile app