Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi wa Kuishi nao milele,
Pongezi kwa watoa elimu na wachangiaji wa kawaida hadi kufikia hapa,
Asanteni sana,

Tiba
kipande cha mti wa muhogo ukiwa safarini hasa zile safari za miguu hakikisha unashikiria mkononi pia usithubutu kubadilisha mkono hiyo ni tiba kwa watu wabaya uwapo safarini,
Lakini kama safari yako si ya miguu basi pata kipande weka mfuko wa suluari au sketi au gauni lako.


Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana,naongeza tu, Kata vipande saba vya mti huo, chemsha jikoni kwa maji, yaepue tumia kumkanda mwenye shida ya kiuno na mgongo!
 
Uzi wa Kuishi nao milele,
Pongezi kwa watoa elimu na wachangiaji wa kawaida hadi kufikia hapa,
Asanteni sana,

Tiba
kipande cha mti wa muhogo ukiwa safarini hasa zile safari za miguu hakikisha unashikiria mkononi pia usithubutu kubadilisha mkono hiyo ni tiba kwa watu wabaya uwapo safarini,
Lakini kama safari yako si ya miguu basi pata kipande weka mfuko wa suluari au sketi au gauni lako.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mti wa muhogo huu tunaochimba na kula au ule usiochimbwa mihogo yaan unao chumwa mboga tu
 
Nisaidie dawa ya jino
Tafuta tangawzi mbichi,kitunguu sawaum na karafuu.

Chukua kipande chá tangawizi kikoshe vizur,Chukua punje 10 za karafuu na punje 4 za kitunguu sawaum vile vidogo vidgo sio vile vikubwa.

Saga kwa pamoja vyote chukua mchanganyiko huwo weka na zungushia sehem ya jino linalouma sehem yote ya jino hadi kwenye ufizi ndani na nje ya ufizi panapouma tumia siku 4.

Mda mzur weka ukitaka kulala ili dawa idumu kwa masaa mdomoni.

Note: dawa hiyo inawasha sana uweze kustahamili sana tena sana kabisa.


Baada ya siku yapili Baada ya matumizi unaweza ukafanya ukungu mweupe na kama mchubuko flan hivi usihofu Baada ya kumaliza tiba na hilo tatizo litapotea wenyewe.

Jitahidi kila mda unaotakakufanya dawa itumie yote kwa wakat huwo na siku ya pili utafanya nyengine fanya kiasi tu yakuwez kukutosha kwa mda huwo.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Poleni na majukumu. Niwapongezi watalaam wetu wanaotupa elimu humu. Mimi naomba msaada wenu kuhusu tiba ya sickle cell au seli mundu. Natanguliza shukrani.
 
Tiba ya korodani mmoja kuwa chini
Mkuu malembeka18; Korodani hazikai hata siku moja mkao wa kulingana (Level). Kwa kawaida na ndivyo tulivyoumbwa, moja huwa juu kidogo ya mwenzake (zinapishana uning'iniaji wake).

Samahani lakini kwani sijajibu hoja yako ya kutaka Tiba ila nimeona nikutoe hofu. Wanaume wote tuko hivyo. Labda kama imezidi mno kiwango chake au kuna maumivu. Asante
 
Ngoja nikapata picha yake nitaliweka ni kama Hilo alilotuma jamaa ila lenyewe linaota lenyewe sio la kupandwa
Hili alovera nimekuta porini ila ni chungu sana nimelitafuna nikashidwa nitofauti na lile la kurudisha kumbukumbu.
IMG_20220809_162058_592.jpg
 
Kuna baadhi ya dawa nimefanya kama mlivo elekeza humu but matokeo yamekuwa ni zero hivyo basi nashauri kuwe na ushuhuda kwa waliofanikiwa kwa dawa walizo elezwa humu, Tusijaze uzi tu humu kwa dawa ambazo hakuna anayezifanyia kazi, Karibuni
NOT, hii nimetoa si kwa kupiga uzi huu.
 
Kuna baadhi ya dawa nimefanya kama mlivo elekeza humu but matokeo yamekuwa ni zero hivyo basi nashauri kuwe na ushuhuda kwa waliofanikiwa kwa dawa walizo elezwa humu, Tusijaze uzi tu humu kwa dawa ambazo hakuna anayezifanyia kazi, Karibuni
NOT, hii nimetoa si kwa kupiga uzi huu.
Mfano?
 
Wakuu natanguliza shukrani na habarini za jioni naombeni dawa ya tumbo kujaaa I'we nimekula sijala lenyewe linajaa tu ata nikila kidogo linajaa
 
Majani ya muhogo,
kingine pilipili,
Nilifanyia kazi vitu vingi, ila nawe angalia kazi ya vitu hivyo kavifanyie kazi harafu leta mrejesho
Ukisema hivyo unakuwa bado hujaeleweka. Elezea vizuri ulitumia muhogo au pilipili kwa njia ipi na ulikuwa unategemea kupata matokeo gani ili ijulikane wapi hapakuwa sawa.
 
...Mwenye kuufahamu mti huu tafadhali...
Kuna dawa fulani ya mtu aloungua na
moto, uwe umetokana na uji,chai au vyovyote vile,
Nakumbuka bibi yangu alikuwa anabandua magome ya mti huo kisha baadhi anapata unga na magome mengine anachemsha kwa kuongeza na maji na baada ya mchemsho huwa na rangi nyekundu kama damu, maji haya ni kwa ajili ya kusafishia vidonda tu na
ule unga wa magome uliosagwa ulikuwa na rangi nyekundu au pinki fulani na hutumika kupaka sehemu zote zilizoungua na moto kisha mgonjwa anaweza kukaa kama siku tatu hivi anaangaliwa kidonda kinaendeleaje ili kufahamu kama kuna ulazima wa kuosha tena na kubandika upya dawa,
KUMBUKA
ya maji ya kusafishia uwe unapasha joto kutokana na uvumilivu wa ngozi ya mtu unaemtibia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida dawa zingine tunazijua kilugha kulingana na kabila husika..
 
Hili alovera nimekuta porini ila ni chungu sana nimelitafuna nikashidwa nitofauti na lile la kurudisha kumbukumbu.View attachment 2319163
Lenyewe sio chungu bwana Kwa sababu mim nimetumia sio kwamb napewa stori na mtu afu ilo lilitaka kufanana na Yale ya kupanda afu ukilimega linamaji mengi litamu halina uchungu kabisa mim nikipata picha nitakutumia ulinganishe na Hilo linaweza likawa Hilo ila likawa limeathiriwa na Hali ya hewa au limekaa mda mrefu ila pia hata Hilo chungu ni dawa ya tumbo hasa tumbo la kuendesha
 
Uzi udumu milele,
Majani ya muhogo,
kingine pilipili,
Nilifanyia kazi vitu vingi, ila nawe angalia kazi ya vitu hivyo kavifanyie kazi harafu leta mrejesho

Kwa jinsi nilivyosoma kupitia huu uzi hayo majani na pilipili ni katika kuleta bahati/ kusafisha nyota.

Umefuata utaratibu wa dozi au formula yake jinsi inavyopasa kutumia,hata chumvi mawe ukiitumia vizuri inatoa majibu ie mara (asbh mchana jioni) 7, 14 au 21 kulingana na ukubwa wa tatizo lako.

Tuondoe mind set kwamba vyetu avina maana kumbuka wazazi/ mababu zetu walisavaivu century na century wakitumia izi formula.

Ivi vitu vinafanya kazi kweliii sema sisi tunataka majibu ya hapo kwa hapo bila kuangalia tatizo mpaka ukaligundua ni kwamba uko nalo muda mrefu ivyo kuliondoa pia itachukua muda.
 
United ya Ferguson

Ulitoa angalizo kuhusu unga wa msamitu.

Nimeona huko facebook madalali wa unga wa msamitu wanauuza kwa pakiti ambayo utatumia wiki 4+. Wengine 37,000/= mpaka 40,000/=.
 
Back
Top Bottom