Habari za usiku huu, naomba nishare nanyi dawa Moja itokanayo na mmea uitwao leaf of life, sijui kwa kiswahili unaitwaje.
Hili Jani nililifahamu kabla lakini sikuwahi kulitumia, Juzi wife alipata tatizo la kifua alikuwa anakohoa Sana, na pumzi zinabana Sana na akipumua ni Kama mtu mwenye pumu, kumbukumbu ikanijia kuwa huu mmea unasaidia kwa matatizo ya upumuaji na bahati ninao mmea wenyewe, nilichuma Jani Moja akalitafuna na kufyonza maji yake, basi baada ya Kama dakika Tano tu akawa Safi kabisa kifua kimefunguka na akapata usingizi Safi kabisa.
Tuutumie huu mmea nasikia umejaaliwa kuwa sababu ya kuponya maradhi mengi tu.
Tafadhali Kama Kuna anayejua matumizi zaidi ya LEAF OF LIFE ni vyema ayaweke ubaoni hapa ili sote tuelimike.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app