Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Watalaamu mi naomba dawa ya kuzuia jipu yani lipotee lisiive, nshatokea jipu nikakamua hospital lakini linarudia tena....hapa leo najisikia tena dalili 🥺 naombeni kama tiba ipo

BIN NUN Crocodiletooth et al please
Mi naona waganga wanahamishaga majipu mfano kama lipo kwenye kali.o linaletwa mguuni kisha linakaushwa
 
Watalaamu mi naomba dawa ya kuzuia jipu yani lipotee lisiive, nshatokea jipu nikakamua hospital lakini linarudia tena....hapa leo najisikia tena dalili [emoji3064] naombeni kama tiba ipo

BIN NUN Crocodiletooth et al please
Pole sana Evelyn Salt. Maelezo yako yanaonesha una mchafuko katika damu ambao husababisha majipu. Hii inatokana na dawa za hospitali unazotumia, vipodozi na vyakula.

Hivyo unapaswa kufanya yafuatayo:
1) Dawa za hospitali unapotumia uwe unakunywa maji mengi
2) Kuwa makini na vipodozi unavyotumia
3) Usile kabisa vyakula vinavyotengezwa kwa ngano (chapati, mikate, biskuti, nk)
4) Usile na kunywa vyakula vilivyotengenezwa viwandani km juisi, vinywaji baridi, nk
5) Usile vyakula vyote vitokanavyo na wanyama au maziwa
6) Usitumie dawa za kutuliza maumivu, dawa za presha, au sukari
7) Usile chakula baada ya saa 2 usiku.
8) Usile virutubisho
9) Usitumie sukari au glucose
10) Kuwa na mazoea ya kumeza kitunguu saumu usiku wakati wa kulala
11) Katakata kitunguu maji, kiweke kwenye kisahani na ulale nacho chumbani kila siku. NB: Ubadilishe kila siku

Kusafisha damu unatakiwa kuchukua majani ya muarobaini na kuyachemsha vizuri kisha kunywa maji yake kikombe cha chai kutwa mara 2 kwa siku 5.

Nasubiri mrejeshonyuma. Kila la kheri
 
Ahsante sana hicho kitunguu maji kinasaidia nini? Hamna dawa sasa ya kulimaliza? Mbali na hayo maelekezo ya kusafisha damu??
 
Ahsante sana hicho kitunguu maji kinasaidia nini? Hamna dawa sasa ya kulimaliza? Mbali na hayo maelekezo ya kusafisha damu??

Kitunguu maji husaidia kuua bakteria wanaoishi vyumbani mwetu kutokana na vumbi pamoja na hewa chafu ya jasho na ushuzi tunaotoa wakati tumelala. Kimsingi kitunguu maji ni "natural antibiotic" na inapendekezwa kukila kila siku kama kachumbali pamoja na nyanya.

Hakuna dawa yoyote duniani, iliyotengenezwa mahabara humaliza tatizo la ugonjwa wowote zaidi ya kufisha nguvu za kinga ya mwili. Vyakula na hali ya maisha ya mwanadamu ndiyo chanzo cha magonjwa mengi kwa kuwa hupunguza nguvu ya kinga mwilini.

Kama ulikuwa hujui, mwili unapopata ugonjwa, Mungu aliuumba kujitibu na kujenga kinga ya ugonjwa huo. Kwa sababu ya mabadiliko katika maisha ya binadamu (ambaye viungo vyake vyaweza kuishi miaka 120) tumeharibu mfumo wa kinga.

Pamoja na yale niliyoeleza hapo awali, yafuatayo yatakusaidia kuongeza kinga ya mwili:
1) Jitambue na kujiamini ukimtegemea Mungu
2) Fanya zoezi kila siku la kutoka jasho (km kwa kutembea). Jasho ndiyo njia pekee ya kuondoa sumu kwenye damu wakati kinyesi na mkojo ni uchafu wa mwilini tu.
3) Kunywa maji mengi hasa kila mara unapotoka haja ndogo kurejesha maji uliyopoteza. Kufanya hivyo kunaimarisha mirija inayosafirisha damu mwilini isisinyae. Kumbuka kuwa damu ndio njia kuu ya kusafirisha hewa safi na virutubisho kwenye mapafu na viungo vyote mwilini.
4) Kula matunda kwa wingi, hasa asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Matunda yana virutubisho vingi vya kuongeza kinga mwilini
5) Pumzika ya kutosha (kwa maana ya usingizi), siyo chini ya saa 5 kwa siku.

Kila la kheri
 
Msaada kwa anayejua dawa ya masundosundo/ vipele sugu chini ya kisogo kutokana na kunyoa, hii huathili sana wanaume. Msaada tafadhali

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
Screenshot_20230710-192451.png
 
Msaada kwa anayejua dawa ya masundosundo/ vipele sugu chini ya kisogo kutokana na kunyoa, hii huathili sana wanaume. Msaada tafadhali

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
Kuna ile miba inayopatikana mbugani kwa Tabora wanaita mang'ombe chukua mwiba ukatie kwenye sundosundo lako utaona linaanza kupukutika lote[emoji120]
 
Back
Top Bottom