Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Mibono ni miti fulani ivi inakua inatoa vitunda lakini haviliwi sana hutumia waislamu Kuwekea kwenye makaburi pindi wakizikana. Ukigoogle tu utaiona mkuu
 
Mibono ni miti fulani ivi inakua inatoa vitunda lakini haviliwi sana hutumia waislamu Kuwekea kwenye makaburi pindi wakizikana. Ukigoogle tu utaiona mkuu
Huu ndio mbono au Mibono?
 

Attachments

  • FB_IMG_1699267196791.jpg
    FB_IMG_1699267196791.jpg
    39.7 KB · Views: 28
Anaejua dawa ya biashara hasa kuvuta wateja dukani ashee nasi au aje pm.
Nipo tayari kuchangia kiasi kidogo kulipa wema wako utakaokuwa umenifanyia. Kikubwa iwe dawa ya uhakika.

Au kama wewe ni mfanyabiashara wa duka na unajua mambo fulani fulani ya kuvuta wateja naomba uje pm tubadirishane maarifa. Naweza kukupa kitu amazing sana
 
Mmea gan?? Huu nmeambiwa unatibu magonjwa mfumo wa mikojo mwenye ujuz.....atupe shule
IMG_20231108_182346_999~2.jpg
 
Anaejua dawa ya biashara hasa kuvuta wateja dukani ashee nasi au aje pm.
Nipo tayari kuchangia kiasi kidogo kulipa wema wako utakaokuwa umenifanyia. Kikubwa iwe dawa ya uhakika.

Au kama wewe ni mfanyabiashara wa duka na unajua mambo fulani fulani ya kuvuta wateja naomba uje pm tubadirishane maarifa. Naweza kukupa kitu amazing sana
Uelekezweje bila kufika kwa mtaalam husika? uko mkoa gani?
 
Picha namba 1,515 hapo juu ni mmea wenye dawa safi sana ya kisukari. Tengeneza chai yake anywe asubuhi na jioni hata Kwa wiki moja
Mi naomba nitumie hiyo picha ya huo mme, nimejaruibu kutafuta sijauona kwa picha.
 
Kama una ndugu amelishwa limbwata lile mume anakuwa zoba, hana sauti, fanya hivi.

Ingia kwenye Banda la kuku, fagia uchafu (kinyesi) kwa kutoa nje.
Okota punje chache za kinyesi cha kuku kisage sana,changanya na maji au kinywaji chochote halafu mpe mlengwa anywe.
Atatapika vibaya mno,akitoka hapo mke atachezea kisago cha mbwa mwizi
Akiua itakuwaje ?
 
Wataalamu ninaomba formula au dawa ya mtu kuacha pombe .Nia yangu nikijua niitengeneze niwasaidie vijana wanaoumiza sana familia zao kwa ulevi.naambiwa ipo mitishamba ambayo mtu anaacha kabisa pombe.Tatizo hawa vijana ni hohe hahe hawana hela za kuona waganga wakubwa wapone .
 
Ndugu wanajukwaa wenzangu,ninawasalimu kwa jina la JMT! Kwa wale ambao Mungu anaendelea kuwajaalia afya njema basi ni jambo la kumshukuru Mungu,lakini pia kwa wale ambao wana matatizo mbalimbali ya kiafya si wakati wa kukata tamaa,kwani siku moja unaweza kupata uzima wako,kikubwa ni kumtumainia yeye aliye juu.

Kuna watu wengi sana wanasumbuliwa na tatizo la bawasili na hata hapa jukwaani wamekuwa wakilalamika sana juu ya adha kubwa wanayoipata kutokana na ugonjwa huu ambao unasumbua sana jinsia zote mbili.

Watu wengi wamekuwa wakiongelea sana chanzo chake na namna ulivyo,kwa hiyo sitajikita kueleza mambo yaleyale ambayo yanaandikwa kila siku.

Kwa wewe unayesumbuliwa na tatizo hili na yawezekana umepita sehemu nyingi bila mafanikio,yawezekana tiba hii ikakusaidia na ukarudi hapa kutoa ushuhuda acha kupuuza.Najua dawa ni code ya mtu kwa ajili ya kipato chake na hata kwangu pia,lakini nimeamua kufanya makusudi ili japo nisaidie wahitaji maana nawahurumia sana.

Tafuta mti unaitwa mjafari,chimba mizizi yake(Nilishawahi kuuandika hapa) kwangua maganda ya mizizi yake vizuri na uyaanike sehemu isiyokuwa na jua kali ili kutokupoteza ubora wake (mzizi wake ni mkali,ladha ya tangawizi na uchungu mkali ndani yake).Baada ya kukauka vizuri,tafuta sufuria uikaange mpaka iingue kama mkaa,baada ya hapo saga vizuri uwe unga mweusi kama wa mkaa.

Tafuta kuna nta ya miti inaitwa DEMOAI ukiingalia vizuri inafanana na asali ikiwa kwenye chupa,ni maarufu kwa jina hilo bila shaka ni kimasai maana wao ndiyo wanaiuza sana,ingawa wanaichakachua kwa kuiongezea mafuta ya kula ili iwe nyingi kwa hiyo inaathirika na kutokuwa na ubora unaotakiwa,kama unaweza kupata pure kabisa ni jambo jema.Hii inapatikana kwenye mapori ya Morogoro,Arusha na hata pwani kidogo,lita moja inaweza kuuzwa zaidi ya laki moja.

Chukua kiasi kidogo cha unga wako wa mjafari ulioundaa kama nilivyoelekeza ( nusu kijiko kwenye kiganja) changanya matone mawili ama matatu ya nta (DEMOAI) changanya vizuri ichanganyike tayari kwa kupaka sehemu yenye tatizo.
Hakikisha unapaka mara mbili kwa siku.

Kama unakuwa na tatizo la kinyesi kigumu tumia matone yasiyozidi matatu ya nta hiyo (DEMOAI) kwenye kikombe kizima cha chai ukoroge vizuri kila siku asubuhi hutajuta tena kujisaidia huku ukitibu bawasili kwa mtindo huo wa kupaka.

Kama bawasili ni za ndani,kuna mti maarufu sana sisi wasukuma tunauita NSUHA( nilishawahi kuandika miujiza yake hapa) huu ni maalum kwa kutoa vimbe za aina zote mwilini unapochanganywa na aina nyingine ya mimea.Tengeneza unga wa mizizi yake na utatumia kijiko kimoja katika maji moto mara tatu kwa siku.

Note: Tiba hii inawasaidia watu wengi na wengi wamepona kabisa.Acha kuzarau mitishamba.Ukipona kumbuka kutoa sadaka kwa Mungu wako.

Ahsante!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kuna watu mbinguni ni kwenu
 
Back
Top Bottom