1.Ujana wako uliutumiaje ?
2.Umri wako uliutumiaje ?
3.Mali yako uliipataje na uliutumiaje ?
4.Elimu yako uliotumia vipi ?
5.Kila mchunga ataulizwa kwa kile alichokichunga
1.Wakati wa ujana mtu anakua na nguvu kubwa kama madhambi basi mtu huyaendea kwa nguvu zote .Mtu akitumia ujana wake vizuri kwa kuchunga mipaka ya Allah ni neema kubwa kuna malipo makubwa sana sababu nguvu na uwezo ulikuwa nao ila ukapiga chini matamanio maovu kwa kumuogopa Aliye kuuumba.
2.Haukupata muda mrefu wa kuishi kiasi cha kukumbuka Kesho yako ?Ni ajabu mno mtu kufika mpaka utu uzima na umri mkubwa mpaka anafariki bado yupo katika wimbi la maasi hapo Unaingia surat_Takathur(102) mtu mpaka anaingia kaburini bila kuwa na kitu chochote cha kumsaidia.
3.Kwenye mali hapo ndio mtihani mkubwa wa umma huu maana mtu yupo tayari afanye lolote ilimradi tu apate pesa bila kujali njia gani ametumia kuipata na wengine kutumia katika matumizi maovu na kusahau wazazi,ndugu,mayatima na wasiojiweza .Sasa hivi kamari imejua maarufu tena kila siku inakuwa kwa majina mbalimbali kama kubeti,korokoro nk
4.Kuna watu wanasoma ilimradi kupotosha watu au wanasoma ili kuwatapeli watu na kuitumia elimu yao kupindisha haki nk
5.Baba na Mama wanajukumu kubwa kuhakikisha watoto wanakua katika misingi imara ili baadae wasiji wakapata kisingizio kuwa tulikuwa tunalelewa vibaya . Vilevile kila mtu ana jukumu kwa kila kinachomzunguka na anachokichunga
Nb: Muhimu kuchukua hatua mapema kuomba msamaha ,toba na dua ni silaha muhimu mno