Aya ninayoipenda mno sababu inatoa taswira hali ya sasa ya wengi wetu kumpuuza maandishi na makatazo ya Qu'ran japo imebainisha wazi kila kitu . Mwenyezi Mungu atuongeze tushikamane nayo ipasavyo
Moja Kati ya vitu ambavyo vitawaingiza watu motoni kwa wingi siku ya kiama ni Ulimi kwani kupitia ulimi mtu anaweza;Kupotosha ,kusengenya ,kuzungumza uongo,kugombanisha ,kuleta fitna ,kutukana nk.
Na katika hadithi moja Mtume Muhammad (SwallaAllahu'aleyhi wa salam) amesema yeye amemdamini pepo mtu anayechunga ulimi na tupu yake.
Sina gari ,mali wala utajiri ila kunakitu kila nikifikiria najiona napaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu sana tena zaidi ya sana si kingine bali kunijaalia mimi kuwa miongoni mwa waislamu kwani maisha yasingekuwa na maana yeyote kwangu bila uislamu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.