Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

Uzi mtamu sana! Nashukuru sijawahi kupatwa na matukio ya ajabu yaliyoambatana na ushirikina, lakini mengi nimeyasikia, dunia hii ni shida!
 
Hu
hukupoteza esiemji kwel wwakati ukibiringita?
 
Nyumba inahitaji maombezi
 
Nakumbuka nikiwa na miaka kama 9 hivi, nilikuwa na wenzangu 4 tulitoroka shule ile saa nne asubuhi (muda wa chai) tukaenda kuwinda ndege na kuchimba sungura huko Tabora (Kijiji cha Kigwa). Tuliingia porini tena pori zito kabisa lililoshona mpaka tukapotea bila kujuwa tuliingilia wapi, hivyo tukawa tunatembea tu na kutungua ndege huku tukitafuta sehemu nzuri ya kutokea lile eneo maana tulikuwa katikati ya pori na tulikuwa hatujuwi wapi tulipo kwa hiyo tukawa tunafuata mwanga wa jua tu. Kidogo mbele yetu tukaona kitu kama tawi hivi linataka kuanguka mbele yetu, mwenzetu mmoja akawa jasiri kwenda kulikata ili tuchimbe sungura vizuri kumbe alikuwa nyoka anashuka kuja kutukimbiza. Mwenzetu alipofika tu akagongwa mkononi na usoni then yule nyoka alishuka na kuanza kujipanga kutufuata sie...nasi kuona vile kila mmoja wetu akakimbia kivyake maana tulikuwa hatujuwi wapi tulipo. Mbeleni huko kukawa na uwazi fulani hivi, tukasimama na kujikuta tuko wawili tu wenzetu wengine hatukujuwa walikimbilia wapi. Tukawa tunawaita bila kujibiwa, kurudi kijijini tukawatafuta hatukuwaona. Usiku ule wazazi wao na polisi wakawa wanawatafuta na wakaja mpaka pale kwenye ofisi ya CCM kuulizia watoto wengine kama waliwaona wenzetu hao. Usiku wa manane wakaja mapolisi na wazazi wa wale wenzetu na kuhamsha wazazi wangu wakitaka kuongea nami kwani kuna mtu aliwaambia mara ya mwisho wale wenzetu walikuwa na mimi. Nikawaambia ukweli kuwa tulitoroka shule na kwenda kuwinda maporini ndipo tukakimbizwa na nyoka. Kwa kuwa ilikuwa usiku, wakaniacha nilale na asubuhi wakaja kutaka niwapeleke eneo la tukio. Kufika kule tukakuta mwenzetu aliyegongwa na nyoka kafa pale pale. Mbele kidogo tukalikuta chatu limeshiba karibu na pango fulani hivi na shati la shule likiwa ndani ya lile pango just next na huyo chatu. Yule chatu akauliwa na kuchunwa ndipo akakutwa mwenzetu mwingine. Hili tukio lilitokea mwaka 1979, na sitolisahau maishani mwangu kamwe. Nilipigwa sana na Mama yangu ile siku na mama alikuwa ananipiga huku akilia kwa hasira mpaka akashikwa na watu asiniue. Utoto ni janga baya sana kwani watoto wanadanganyana mno.
 
Hata Mimi nawaza hivyo ! iLa jamaa mwenye ile Pete ni kichwa kweli darasani ndio alikua anategemewa, jamaa alikua fundi wa kupiga kinanda ile mbaya, na alikua kiongozi(mwenye kiti) wa kikundi cha (TYCS)

hii story kama naijua, ulisoma shule gani mkuu kama hutojali
 
Aisee ilikuwa nomaa sanaaa
 
Duh pole sana mkuu,kutokana na stories nazoziskia kuhusu mapori ya tabora siku ikitokea hata napita na gari sitashuka kuchimba dawa hata iweje

Huyo nyoka atakua ni koboko tu,najiuliza na huyo alieliwa na chatu sijui alianguka na kushindwa kukimbia tena,au alipoteza fahamu kabisa
 
Aiseee watu mna historia kwakweli, bora hata mie wenzangu walikufa mie tayari nipo huku mjini ila wewe walikufa mkiwa wote. Hii history haiwezi kufutika hadi unaingia ardhini na kwa kuhisi sometimes inakutesa akili
 


Sidhani kama kuna mkoa wenye nyoka wa hajabu ama wingi wa nyoka hapa Tanzania kama Tabora. Ni kweli baadaye iligundulika yule nyoka alikuwa koboko kutokana na mazingira ya pale. Pia polisi walisema inaonekana yule mwenzetu aliyemezwa na chatu alikuwa alilala kwenye pango bila kujuwa kuna chatu kwani waliposachi mle ndani ya pango walikuta mifupa ya wanyama na baadhi ya mayai ya chatu ambayo yalikuwa yametotolewa. Hivyo mwenzetu alivamiwa na chatu na kukunjwa akiwa usingizini kisha kumezwa. Hii kitu kwa kweli inaniuma sana haswa nikifikiria jinsi alivyokunjwa, yaani kuvunjwa mifupa.....ndiyo maana sipendi kabisa nyoka.
 
Aiseee watu mna historia kwakweli, bora hata mie wenzangu walikufa mie tayari nipo huku mjini ila wewe walikufa mkiwa wote. Hii history haiwezi kufutika hadi unaingia ardhini na kwa kuhisi sometimes inakutesa akili


Sikufichi, inanichanganya sana akili wakati mwingine haswa nikiona wasukuma wanavyocheza na chatu....yaani sitaki hata kuona.
 
Poa mkuu, pia avatar yako ni mojawapo ya mambo yanayonitisha niliyowahi kutana nayo mkuu[emoji23]
Mkuu avatar yake huoni km ni picha ya mwanae?ss na mwanae tena ni moja ya mambo uliyowahi kukutana nayo tena!!!!![emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 

Mkuu, tunasubiri Simulizi
 
Duuh mlikutana na black mamba mkuu
Tabora wapo kibaaooo
 
Inatisha sana aisee! Hili tukio sio rahisi kusahaulika maana ulipona kwa neema tu wala sio kwa ujanja wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…