Nakuja na kazi ya kufanyia popote ulipo, kaa tayari.
Update: hii hapa 👇
Tangazo la Kazi: Fursa ya Kuwa Wakala wa Sahili Marketplace Network
22nd Oct 2024
Sahili Marketplace Network inatafuta vijana kutoka karibu kila mkoa wa Tanzania ili kusaidia wajasiriamali kujisajili na kufungua maduka kwenye mtandao wetu mpya wa biashara kwa wajasiriamali nchini. Tunahitaji watu kutoka mikoa ifuatayo:
- Mwanza (3)
- Dodoma (2)
- Dar Es Salaam (3)
- Arusha (2)
- Mbeya (3)
- Morogoro (2)
- Tanga (2)
- Kigoma (2)
- Kagera (2)
- Shinyanga (3)
- Pwani (2)
- Iringa (2)
- Tabora (2)
- Singida (2)
- Kilimanjaro (2)
- Lindi (2)
- Ruvuma (2)
- Mtwara (2)
- Manyara (2)
- Geita (2)
- Njombe (2)
- Mara (2)
- Katavi (2)
- Simiyu (2)
- Rukwa (2)
Kila wilaya itapata mawakala zaidi kulingana na mahitaji yanavyoongezeka hapo baadaye.
Kuhusu Sahili Marketplace Network:
Sahili Marketplace Network ni jukwaa la kipekee linalowaleta pamoja wajasiriamali wa Tanzania.
Ni soko la mtandaoni ambapo watumiaji wanaweza kuuza na kununua bidhaa, kujadili na kutoa maoni, pamoja na kupata makala na blogu za kijasiriamali. Tunahimiza ubunifu na tunatoa fursa kwa wajasiriamali wa bidhaa za asili na za kienyeji kuwa sehemu ya mtandao huu. Tunasisitiza hii ni kwa wale wanaozalisha bidhaa zao iwe ni kibinafsi au ni kiwanda kidogo, cha kati na hata kikubwa.
Malipo:
- Malipo ni kwa mfumo wa kamisheni (%). Kwanza, utasajili watu watano bure bila malipo, kisha utalipwa kwa kila mtu wa ziada utakayemsajili (pendekezo ni TZS 1,000 kwa kila mtu). Kwa mfano, ukisajili watu 25 kwa siku, utapata TZS 25,000.
- Kipengele hiki cha watu watano wa kwanza kimewekwa ili kuepuka mawakala kujisajili wenyewe au kudai malipo bila kusajili wajasiriamali halisi.
Kumbuka: Kila mjasiriamali anakaribishwa kujisajili. Kujisajili kwa mjasiriamali yeyote ni BURE halipwi wala halipii (maana hawajavuka watu watano). Wanaolipwa ni hao mawakala watakaowasaidia kujisajili. Kwa hivyo wewe mjasiriamali ambaye tayari unauza bidhaa zako Sahili Marketplace Network, unakaribishwa kuwaalika wajasiriamali wenzako kujisajili. Kumbuka katika 'nanenane effect' tunauza zaidi kadri tunavyowapata watu wengi zaidi kuhudhuria maonesho haya ma mtandaoni. Ukivuka watu watano unastahili kupokea comission% ni kusema tu, mimi fulani duka langu ni fulani, nimemsajili 12345678910.
Majukumu ya Kazi:
1. Kusajili wajasiriamali binafsi wanaouza bidhaa walizotengeneza wenyewe kwenye mtandao wa wajasiriamali Tanzania. Hawa wanaweza kuwa wabunifu, wataalamu wa tiba asilia, na wajasiriamali wengine.
2. Kwa kila unayemsajili, kumfungulia duka na kuweka bidhaa mbili au zaidi katika maduka yao. Tunapendekeza kila duka liweke bidhaa si chini ya nne ili kuboresha muonekano wa duka kwenye mtandao.
Sifa Zinazohitajika:
1. Ujuzi wa kutumia simu au kompyuta na intaneti.
2. Uelewa wa jinsi ya kutumia mtandao wa Sahili Marketplace (utapatiwa kipeperushi cha mwongozo).
3. Uwezo wa kuwapata wajasiriamali wenye sifa zinazostahili, ambao wana barua pepe, ni Watanzania, na wanatengeneza bidhaa zao wenyewe mbalimbali. Nakupa mfano wa katika picha hii:
Faida:
- Wakala atakayefanya vizuri anaweza kuajiriwa kama mtoa huduma kwa wateja na kufanya kazi kutoka nyumbani (remote work) kwa malipo mazuri.
- Kufanya vizuri kunakozungumziwa sio idadi pekee bali ni ubora wa watu unaowasajili, ubora wa maelezo mnavyoyaweka na ubora wa picha mnazopiga kiufupi 'Quality is the code we live by'
Jinsi ya Kuanza:
- Kwa mawasiliano na maelezo zaidi, tafadhali tuwasiliane kupitia PM au WhatsApp 0734189022 kabla ya kuanza kazi.
- Ili kuepuka kuwa na mawakala wengi kwenye mkoa mmoja, tafadhali uliza kwanza kama nafasi ipo kwa mkoa wako kwa kusema, "Nipo mkoa X, nataka kuanza kazi, je nafasi ipo?"
Mwisho wa Kuomba (Deadline):
Wiki moja baada ya tangazo hili kutolewa.
Jiunge nasi sasa, kuwa sehemu ya mapinduzi ya biashara ya mtandaoni Tanzania kupitia Sahili Marketplace Network!