Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Ila kuna watu mnahangaika aisee. Au ndo nyie mkija huku mnasema hamna Mungu. Aisee mtegemeeni Mungu jamani huku ndiko kwenye suluhisho
Na ajabu ,Bado wanatafuta waganga
Meaning hawajafanikiwa!
Ushirikina haijawahi muacha mtu salama,ye na familia
 
Kuna watu mpaka wananukia kiganga kiganga nsiwataje ila kashajijua.
 
Kabisa waganga ndo wezi wa nyota za watu wanaoenda huko
 
Na wanawake sikuhizi wameshtuka
Nao washirikina balaa sbb wako kifedha
So,Ngoma droo!
Hakika , uzinzi na uasherati ni mbaya sana
 
Mnapoteza Muda tu
Mafanikio hamna
Maisha Magumu hayaishi
Haya mambo siamini kwa sababu tuu mazingira niliyokua na kuaminishwa uganga ni kitukibaya, lakini haya ndio mambo mababu zetu walikuwa wakifanya, mkoloni kaja katurisha sumu basi kila kitu chetu ni kibaya, mkoloni alituondoa kwenye reli na inawezekana kabisa babu zetu walikuwa na vitu vizuri kabisa
 
Logically hao wote watakua waongo. Sababu kama umekutana na "A" na akawa mzuri basi usingekua na haja ya kwenda Kwa B, C, D au E.

Au kama A alikua muongo ukaja kukutana na B mkweli basi ungeishia hapo hapo kwe B ukawa unamtumia tu huyo huyo
Kwa hiyo wewe ukila pisi kali ndio umemaliza na hutaki nyingine tena?
 
Kuna Mganga maeneo haya ya Nkome Geita anaitwa Mariam, huyu mama ni bigwa wa jutibu vichaa, binafsi kuna mtu wangu wa karibu alitibiwa kwa muda mfupi sana.
Nkome maeneo gani
Mtoto wa shangazi anmechanganyikiwa
Yupo katoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…