Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

LEO naomba Tuwasaidie wale ambao nauli za kwenda mkoani Hawana , Hivi Kuna Waganga wakweli dar au bagamoyo ? Kama unamjua taja jina na Mahali anapopatikana Haina haja ya Mawasiliano Anayehitaji Atamtafuta.
Mi natafuta mganga wa utajiri hata kama nitaishi muda mfupi ili afanikishe lengo la kuwa tajiri nipo serious mkuu.

Masharti yoyote nipo tayari kasoro la kutoa kafara ndugu wa karibu.
 
Huu Uzi Maalumu wa Kupeana Connection Za Waganga wa Kienyeji na Shuhuda Mbalimbali.

Kikubwa Toa Shuhuda Elezea Location Alipo Mawasiliano sio Muhimu kwa Kuwa watembeaji ni Watu wa Kujiongeza.

Nitaanza mimi.

1. Mganga wa Kwanza Nilikutana Naye kigoma Huko wilaya Ya Kakonko , Alikuwa Mama wa Makamo Mwenye Mguu Mbovu , Yule Mama Alikuwa Kiboko Aisee Akikufanyia Jambo Lazima lishike.

Kwanza Ukifika Kwake Kazi Anafanya Asubuhi tu Saa 12 mpka sa4 mwisho , Ukiingia Tu Unakutana na Kitambaa Ukutani kama Kuna Wabaya waliowahi kukufanyia kitu kibaya wote utawaona pale na vitu vyote walivyokufanyia , Mkishaangalia pamoja ndio Anaanza Matibabu.

Huyu ndiye aliyenifanya niamini baadhi ya Mambo tunayo yaonaga kwenye muvie za Kinigeria kuwa Yapo . Alikuwa kiboko sanaa kwa maradhi ya kimwili na wale wanaotaka hela za masharti . Kwa bahati mbaya mwaka jana niliambiwa amekufa kamwachia mtoto wake sijajua kama huyo mtoto atakuwa balaa kama Mama yake.

2. Nikajongea maeneo ya Biharamulo huko Nilikutana na Fundi ambaye anapiga Ramli Usiku yani huyu ni kiboko ya Wasiri , Nikienda pale akianza ramli anauwezo wakumuita mtu yoyote popote Alipo atakuja na Atatoa siri zote yaani ataongea kila kitu . Huyu nilikutana na baadhi ya viongozi wanaofichuaga siri za watu ila huyu mganga naye nilimwamini kwa kiasi fulani ingawa sikupata tiba kwake mana nilienda kuwasikiliza na kuwaita baadhi Ya watu.

3. Kuna mmoja Nilienda kwake Aisee huyu yeye nilimuona hamna kitu alikuwa maeneo ya Ukerewe kwanza picha inaanza kila alichoniambia alinambia vitu ambavyo sijawahi fanya wala kunikuta ila akawa anakomaa kuwa hayo ndo matatizo yangu yule mzee nilimkubalia ila nilivotoka sikurudi kabisa.

4. Kuna Mganga Nilikutana Naye maeneo ya Bagamoyo ni shehe yeye anatumia visomo binafsi sio muumini sanaa wa kusomewa kwani naona ni sawa tu na kuombewa unaweza fanikisha au usifanikishe , Yule mzeee Alinipeleka baharini Tukavunja nazi na Kusoma Dua zao zile ila yule kilichonipeleka sikukufanikisha Japo wenyeji walikuwa wakimsifia sanaa.

Nishakutana na waganga wengi mpka wa Dar es Salaam wakweli na Waongo ila Asikudanganye mtu Ukiamua kuamini waganga wapo watakaokusaidia na wapo watakaokupoteza kikubwa ni Kuwatambua tu , Uzuri ukishakuwa mtembeaji sanaa Huwezi Danganywa kinjinga.

Mi ngoja niishie hapa wengine endeleeni mtoe mliyokutana nayo kwa Waganga huko , saivi natafuta connection ya Kwamsisi kuna mambo nataka nikawaone Nao Ujuzi wao
kaziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ipo
 
Najua wengi watadharau ila mimi niliingia hizi mambo baada ya fala mmoja kunivunjia ndoa yangu alikuwa msela tu yuko TRA si unajua mikwanja njenje akapita na mama Vero wangu mpaka akavunja ndoa niliumia sana afu Kijana alikuwa Tycoon nilimwendea magomeni tu sio mbali si watu wanasema Dar hakuna waganga ?? Acha bhana ilifanyika kazi kwanza yule kijana aliandika barua ya kuacha kazi mwenyewe imegine mshahara wa M3 na zaidi sasa hivi kachoka vibaya sana anasimamia vibanda vya chips
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16] Daaaahh life hili ni balaaahh
 
Sasa sikieni,
Kuna mtu amenidhulumu kama 40mil hivi. Nataka anirudishie hii hela au aondoke tu nikadai changu msibani.

Ila kitu kimoja Kwa Sasa sina hela ya kumlipa mganga hivyo nikilipwa hizo nazodai ndio nitatoa humo humo ya mganga pamoja na ahsante kwa atakaeniunganisha.

Mwenye anajua hii issue ina solvika vipi karibu DM.

NB
Mdaiwa wangu anaweza nae kua ni mshirikina hatari pia hivyo mtaalam wa hii mambo awe yuko vizuri tu.
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh
 
Tatizo tukiweka namba zao wengi watajua ni promo ila waganga wapo wanatibu hadi HIV kwa makubaliano unatibiwa unakaa mwaka baada ya kupona ndio unalipa hakuna utaperi wala nini
Wa wap unaye mkuu ? Kama ni Geita nitajie KIJIJI Tu na jina la mtaalamu
 
Siku ya 9 leo niko kwa mganga mmoja bibi kizee asiyetoka kitandani maeneo ya sengerema hapa.

Nikiona matokeo ntawapa ramani ila mambo yake si haba
IMG_20230815_132431_047.jpg
 
Kama unahakika kadhurumu hata awe mshirikina vipi bro kuna mzee moja hapo magomeni ni hatari anamfanyia hafi ila utamwona tu atachoka kiuchumi balaa hadi utamwonea huruma
Huyo wa kuchoka ki uchumi nitalipwa vipi Sasa. Anatakiwa apate janga ili ndugu zake na yeye mwenyewe wajichange lisiwakute baya zaidi
 
Back
Top Bottom