Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Mpaka kesho PM yako itajaa maombi ya namba ya Kakonko hasa toka kwa kina dada.

Ukijipanga vizuri ni fursa nzuri ya kupata pesa ya vocha.

Wapo wengi hapa watacomment kupinga ushirikina lakini baadhi wana hirizi kwenye mapochi, chale mpaka matakoni na wengine ndio wanatoka kupiga ramli saa hizi.
Hiyo ndiyo imani ya kweli ya mwafrika kabla ya kuja wazungu na waarabu hapa Afrika.
Baada ya kuja wamekujaza imani zao (uislamu na ukristo ) wakati wao walikuwa wanafanya biashara ya watumwa, wameua sana ndugu zetu, wamepora mali zetu na kutugawa.
 
Huu Uzi Maalumu wa Kupeana Connection Za Waganga wa Kienyeji na Shuhuda Mbalimbali.

Kikubwa Toa Shuhuda Elezea Location Alipo Mawasiliano sio Muhimu kwa Kuwa watembeaji ni Watu wa Kujiongeza.

Nitaanza mimi.

1. Mganga wa Kwanza Nilikutana Naye kigoma Huko wilaya Ya Kakonko , Alikuwa Mama wa Makamo Mwenye Mguu Mbovu , Yule Mama Alikuwa Kiboko Aisee Akikufanyia Jambo Lazima lishike.

Kwanza Ukifika Kwake Kazi Anafanya Asubuhi tu Saa 12 mpka sa4 mwisho , Ukiingia Tu Unakutana na Kitambaa Ukutani kama Kuna Wabaya waliowahi kukufanyia kitu kibaya wote utawaona pale na vitu vyote walivyokufanyia , Mkishaangalia pamoja ndio Anaanza Matibabu.

Huyu ndiye aliyenifanya niamini baadhi ya Mambo tunayo yaonaga kwenye muvie za Kinigeria kuwa Yapo . Alikuwa kiboko sanaa kwa maradhi ya kimwili na wale wanaotaka hela za masharti . Kwa bahati mbaya mwaka jana niliambiwa amekufa kamwachia mtoto wake sijajua kama huyo mtoto atakuwa balaa kama Mama yake.

2. Nikajongea maeneo ya Biharamulo huko Nilikutana na Fundi ambaye anapiga Ramli Usiku yani huyu ni kiboko ya Wasiri , Nikienda pale akianza ramli anauwezo wakumuita mtu yoyote popote Alipo atakuja na Atatoa siri zote yaani ataongea kila kitu . Huyu nilikutana na baadhi ya viongozi wanaofichuaga siri za watu ila huyu mganga naye nilimwamini kwa kiasi fulani ingawa sikupata tiba kwake mana nilienda kuwasikiliza na kuwaita baadhi Ya watu.

3. Kuna mmoja Nilienda kwake Aisee huyu yeye nilimuona hamna kitu alikuwa maeneo ya Ukerewe kwanza picha inaanza kila alichoniambia alinambia vitu ambavyo sijawahi fanya wala kunikuta ila akawa anakomaa kuwa hayo ndo matatizo yangu yule mzee nilimkubalia ila nilivotoka sikurudi kabisa.

4. Kuna Mganga Nilikutana Naye maeneo ya Bagamoyo ni shehe yeye anatumia visomo binafsi sio muumini sanaa wa kusomewa kwani naona ni sawa tu na kuombewa unaweza fanikisha au usifanikishe , Yule mzeee Alinipeleka baharini Tukavunja nazi na Kusoma Dua zao zile ila yule kilichonipeleka sikukufanikisha Japo wenyeji walikuwa wakimsifia sanaa.

Nishakutana na waganga wengi mpka wa Dar es Salaam wakweli na Waongo ila Asikudanganye mtu Ukiamua kuamini waganga wapo watakaokusaidia na wapo watakaokupoteza kikubwa ni Kuwatambua tu , Uzuri ukishakuwa mtembeaji sanaa Huwezi Danganywa kinjinga.

Mi ngoja niishie hapa wengine endeleeni mtoe mliyokutana nayo kwa Waganga huko , saivi natafuta connection ya Kwamsisi kuna mambo nataka nikawaone Nao Ujuzi wao
Logically hao wote watakua waongo. Sababu kama umekutana na "A" na akawa mzuri basi usingekua na haja ya kwenda Kwa B, C, D au E.

Au kama A alikua muongo ukaja kukutana na B mkweli basi ungeishia hapo hapo kwe B ukawa unamtumia tu huyo huyo
 
Umaskini mwingine ni wakujitakia tu, yaani unaamini kwa kupewa connection ya mganga fulani utatoboa maisha?

Mbona mganga mwenye ni choka mbaya tu kila idara ya maisha yake!!?
Hiyo ndiyo imani ya kweli ya mwafrika kabla ya kuja wazungu na waarabu hapa Afrika.
Baada ya kuja wamekujaza imani zao (uislamu na ukristo ) wakati wao walikuwa wanafanya biashara ya watumwa, wameua sana ndugu zetu, wamepora mali zetu na kutugawa.
 
Logically hao wote watakua waongo. Sababu kama umekutana na "A" na akawa mzuri basi usingekua na haja ya kwenda Kwa B, C, D au E.

Au kama A alikua muongo ukaja kukutana na B mkweli basi ungeishia hapo hapo kwe B ukawa unamtumia tu huyo huyo
mtu anahama kikazi kila baada ya mda flani atamtumiaje fundi mmoja tu mkuu?
 
1. Yupo mmoja maeneo ya runzewe bibi fulani kufika kanambia lete pesa pumulia kwenye pesa akanambia matatizo yangu
2. Wapili sasa ni kiboko mnaingia kwenye kijumba anaziba kabisa anaita watu mnakuwa gizan anaita watu wanaongea yeye anawaita wazee ( majini) ni noma na nusu sema yeye hapatikan kwa urahisi ila yupo karibu na boda ya uganda

3. Wa mwisho nae yupo hukohuko ni kijana anaitwa baba love nae ana balaa akichanganya madawa hadi moto unawaka
Ukionaaa likes nyingiii mfwate huyoooo ujue wemye likes wamepishanaaa hukooooooo

Siriyakooo
 
We muanzisha uzi lzm utakuwa ni mganga tu unatafuta promo humu
Waganga wote wa kienyeji ni bahati nasibu na ni hatari kabisa kwa afya yako.
Corona imemaliza watu waliokuwa wapi?
Maradhi yote yanayojulikana hakuna mganga aliyefahamika kuyatibu KITAIFA zaidi ya shuhuda za mitaani tu.

Nendeni Hospital acheni ujinga.
 
Back
Top Bottom