Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

1. Yupo mmoja maeneo ya runzewe bibi fulani kufika kanambia lete pesa pumulia kwenye pesa akanambia matatizo yangu
2. Wapili sasa ni kiboko mnaingia kwenye kijumba anaziba kabisa anaita watu mnakuwa gizan anaita watu wanaongea yeye anawaita wazee ( majini) ni noma na nusu sema yeye hapatikan kwa urahisi ila yupo karibu na boda ya uganda

3. Wa mwisho nae yupo hukohuko ni kijana anaitwa baba love nae ana balaa akichanganya madawa hadi moto unawaka
Si mtaje majina yao
 
Huu Uzi Maalumu wa Kupeana Connection Za Waganga wa Kienyeji na Shuhuda Mbalimbali.

Kikubwa Toa Shuhuda Elezea Location Alipo Mawasiliano sio Muhimu kwa Kuwa watembeaji ni Watu wa Kujiongeza.

Nitaanza mimi.

1. Mganga wa Kwanza Nilikutana Naye kigoma Huko wilaya Ya Kakonko , Alikuwa Mama wa Makamo Mwenye Mguu Mbovu , Yule Mama Alikuwa Kiboko Aisee Akikufanyia Jambo Lazima lishike.

Kwanza Ukifika Kwake Kazi Anafanya Asubuhi tu Saa 12 mpka sa4 mwisho , Ukiingia Tu Unakutana na Kitambaa Ukutani kama Kuna Wabaya waliowahi kukufanyia kitu kibaya wote utawaona pale na vitu vyote walivyokufanyia , Mkishaangalia pamoja ndio Anaanza Matibabu.

Huyu ndiye aliyenifanya niamini baadhi ya Mambo tunayo yaonaga kwenye muvie za Kinigeria kuwa Yapo . Alikuwa kiboko sanaa kwa maradhi ya kimwili na wale wanaotaka hela za masharti . Kwa bahati mbaya mwaka jana niliambiwa amekufa kamwachia mtoto wake sijajua kama huyo mtoto atakuwa balaa kama Mama yake.

2. Nikajongea maeneo ya Biharamulo huko Nilikutana na Fundi ambaye anapiga Ramli Usiku yani huyu ni kiboko ya Wasiri , Nikienda pale akianza ramli anauwezo wakumuita mtu yoyote popote Alipo atakuja na Atatoa siri zote yaani ataongea kila kitu . Huyu nilikutana na baadhi ya viongozi wanaofichuaga siri za watu ila huyu mganga naye nilimwamini kwa kiasi fulani ingawa sikupata tiba kwake mana nilienda kuwasikiliza na kuwaita baadhi Ya watu.

3. Kuna mmoja Nilienda kwake Aisee huyu yeye nilimuona hamna kitu alikuwa maeneo ya Ukerewe kwanza picha inaanza kila alichoniambia alinambia vitu ambavyo sijawahi fanya wala kunikuta ila akawa anakomaa kuwa hayo ndo matatizo yangu yule mzee nilimkubalia ila nilivotoka sikurudi kabisa.

4. Kuna Mganga Nilikutana Naye maeneo ya Bagamoyo ni shehe yeye anatumia visomo binafsi sio muumini sanaa wa kusomewa kwani naona ni sawa tu na kuombewa unaweza fanikisha au usifanikishe , Yule mzeee Alinipeleka baharini Tukavunja nazi na Kusoma Dua zao zile ila yule kilichonipeleka sikukufanikisha Japo wenyeji walikuwa wakimsifia sanaa.

Nishakutana na waganga wengi mpka wa Dar es Salaam wakweli na Waongo ila Asikudanganye mtu Ukiamua kuamini waganga wapo watakaokusaidia na wapo watakaokupoteza kikubwa ni Kuwatambua tu , Uzuri ukishakuwa mtembeaji sanaa Huwezi Danganywa kinjinga.

Mi ngoja niishie hapa wengine endeleeni mtoe mliyokutana nayo kwa Waganga huko , saivi natafuta connection ya Kwamsisi kuna mambo nataka nikawaone Nao Ujuzi wao
Utazunguka sana ila siku ukifika kwa Yesu utatulia.
 
Enheeee..SASA mkuu kipi nafuu, mganga masikini akufanyie mambo yako yanyooke au Pastor Tajiri anaezidi kukukamua hela na hakuna unachofanikisha??
Mada haihusu pastors Ila kama utapenda tuwajadili we anzisha tu uzi.

Tuwajadili kuhusu waganga wa kienyeji aka witch doctors.

Tuendelee na mjadala husika.
 
1. Yupo mmoja maeneo ya runzewe bibi fulani kufika kanambia lete pesa pumulia kwenye pesa akanambia matatizo yangu
2. Wapili sasa ni kiboko mnaingia kwenye kijumba anaziba kabisa anaita watu mnakuwa gizan anaita watu wanaongea yeye anawaita wazee ( majini) ni noma na nusu sema yeye hapatikan kwa urahisi ila yupo karibu na boda ya uganda

3. Wa mwisho nae yupo hukohuko ni kijana anaitwa baba love nae ana balaa akichanganya madawa hadi moto unawaka
Kuwaka moto wala siyo uganga, ni chemical inaitwa pangaline, nenda kwenye maduka wanayouza vifaa vya ulonzi nunuwa hiyo pangaline nenda nayo kwako imwage juwani weka na karatasi ni lazima ulipuke moto mkubwa, Sasa hapo kalumanzira ndio anakuseti kwenye swaga zake.

Hizo ni chemical composition tu.
 
Kuna mmoja alinifanya nifanye mtihani bila ada. Huyu ni kiboko nimetoboa chuo Kwa mbinde sana.
Nilipomaliza Hilo basi sijajihusisha Tena na ishu za shirki[emoji3][emoji3]
Mungu anisamehe tu ni shida zilinielemea
Ila kama unahitaji mawasiliano nicheki pm
Nimecheka sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787] huyo kiboko
 
Ukitafakari kwa makini, wengi waliofanikiwa walipata mganga wa kweli ila wana mbwembwe nyingi "mara Mungu kanijalia" sema hivi kwa ufasaha "Mungu kanijalia kupata mganga wa kweli". Tusidanganyane bwana. Hata hawa jamii ya "Bwana asifiwe mambo ni yale yale".
 
Back
Top Bottom