Uzi wa kupeana shuhuda mbalimbali za Waganga wa Kienyeji

Sema waafrica tumeoshwa bongo zetu na wazungu zikaosheka tunatumia vibaya sana dhana ya neno Mungu, wazungu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutuaminisha kuwa vitu vyetu vyote ni vibaya, wazungu wamekuja Africa haifiki hata miaka 500 wakati waafrica tulikuwepo kwenye bara hili zaidi ya miaka milioni 4 iliyopita history inathibitisha hilo. Kwahiyo mnataka kusema waafrica walikuwa hawamjui Mungu wala hawaabudu? Jiulize kwanin unaitwa James wakati wewe sio mzungu na unaitwa omary wakati wewe sio mwarabu, kwenye imani zetu watu weusi walikuwepo watu waliopewa nguvu na mungu ya kuisadia jamii yao kwenye matatizo flani(kisasa mnawaita the choosen) pia katika jamii walikuwepo watu waliopewa nguvu wakazitumia vibaya so inategemea unaenda kwa mganga yupi kati hao.
 
Umenikumbusha ndugu wa mke wangu walivyokuwa washirikina, yaani tangu nilivyooa ni vurugu za kijinga huku mke wangu akitaka kuondoka kwasababu za kijinga tu, nilipowajua na kupiga biti familia inaenda poa
 
Elezea zaidi
Nimeoa maeneo yaliyo karibu na ndugu wa mke wangu, sasa watu wa huku wanahusda sana, kutokujua na utoto sijui, walikuwa wanakuja nyumbani na kama wanashida nawasaidia, kumbe kinawauma kweli, wakaanza kuniharibia ndoa yangu kila siku kununiana, chokochoko zisizoisha mpaka mke anataka kuondoka wakati mahitaji yote muhimu natoa, ikabidi nikae na staff mwenyeji wa huku ndio akaniambia hauwajui watu hili eneo na usipokuwa makini wataharibu ndoa, ndio nikaanza harakati za kupata tiba mbadala na jamaa akanieleza matukio yote mfano pesa nilitoa kumsaidia mgonjwa ila kumbe nikatengenezewa chuma ulete home, aisee alivyonifungua kwanza walishakata miguu nyumbani pia hata mazoea nikakata, mpaka leo nadunda tu
 
Vipi ela Yako ulitoa akapeleka Kwa mganga au sijaelewa na ilifanyaje kazi bila kukurudishia mkononi
 
Emb elezea hiyo chuma ulete ela ulimpa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…