Nilikuwa sipigwi kama mzee akiwepo ila akitoka naoga vya mbwa koko, nikifanya kosa mzee ananitetea, Mzee alikuwa ananipa nyama nzuri nzuri kama mapaja ya kuku[emoji16][emoji16]..
December nilipata likizo kazini baada ya mia 3 kutoenda nyumbani ile nafika naambiwa kuna mbuzi kwa ajili yako mwanangu(mzee alisema), baada ya mbuzi kuchinjwa siku ya x-mass nikaambiwa chukua nyama uchome tani yako hapo nimeletewa kreti la soda..
Tarehe 26 mzee wangu akaagiza Sato wakubwa hatari kama kichwa cha kiduku Lilo
Mpaka hapa nilipo mzee wangu amenichapa mara mbili tu, ila nilikuwa napewa kichapo heavy kutoka mama.. My mom kwa sasa na yeye ananidekeza hatari na ukubwa wote huu, kiufupi nadekezwa sana dada zangu pia.
Kipindi naanza kazi kabla ya salary kutoka my sister alikuwa anitumia pesa pasipo kumuomba..
Mpaka sasa nadekezwa sana na wazazi na dada zangu ila sio kaka zangu.
Kuwa lastborn raha sana
Sent from my iPhone using JamiiForums