Uzi wa ma-lastborn tu

Uzi wa ma-lastborn tu

Hahaaa ulast born rahaa kweeeli....mimi ikipita mwezi sijaenda nyumbani, mamaa anashangaa atapiga kuniuliza mbona sijaenda kunyonya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mengi yasiwe mambo
Mimi nakumbuka kuna siku kabla sijatoka home dogo alinikuta sebuleni naangalia kideo npo bize hatari flash yenyewe nliazima kwa mwana dogo akaja akabadilisha nkamzaba Kofi akaanza kulia aiseee jinsi ambavyo maneno yalimtoka Bi mkubwa dah jioni kuja kushtaki kwa mzee nikaambulia kuambiwa''kwani luku ulinunua wewe we unafanya kazi hela zako si unakunywa bia nenda kaangalie movie zako huko huko bar''Kidume nikaona ninyamaze mambo yasiwe mengi
 
Na kuwasomesha wazazi wakiwa hawapo


Sent using Jamii Forums mobile app
Na wengine wanasomeshwaga na huku wazazi wapo... Yaani hutu tubwana mdogo tuna shida sana... halafu kwa kulalamika sasa..!!! tunaongoza kulalama hadi kero...

Unfortunately hayo madeko wengine huingia nayo hadi kwenye ndoa... Sasa ukute first born kaowana na last born ..weeeeee..... yaani huyu first born anakuwa si mwanandoa, bali mzazi wa mwenzie... Yaani katoka kulea wadogo zake na sasa analea mwanandoa kama mdogo wake
 
Hakika sisi ni wa kwake (Allah) na kwake ni Marejeo yetu. Pumzika kwa amani mdogo wetu
pumzika kwa amani mdogo wangu ....jana tuu nilikukumbuka , wakati nasikiliza wimbo wa Maroon 5-Memories , nawish ungekuwepo na mimi ningekuwa ninavimba kuwa na kabeauty sibling ,
Mama , kaka zako na dada yako Tumekumiss sana unaishi mioyoni mwetu Forever

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kuchezeshwa kichapo Cha mbwa koko na bro kisa sijaosha vyombo[emoji23][emoji23]
Siku nyengine sijui nilifanyaje akanikurupua usiku ati anitwike mimboko ila limboko lenyewe lile halikuwa fimbo lilikuwa ni likuni nikaona ngoja nitumie nafasi yangu ya uziwanda imtese usiku huohuo nikakimbia kusikojulikana!! Kwani palilalika ni kunitafuta bi maza alimtukana kila tusi halafu wanaenda mpk mbali kunitafuta wkt mhuni nimejibanza jirani nawasikia tu[emoji23][emoji23]

Mziwanda Mimi nilikuwa mmwaga kojo hatari siku moja sista akanifungia kazi asubuhi tu nishachafua mashuka wacha anitimue nikiwa uchi mi nachekelea najiuliza huyu sister leo mbona kanigeukia halafu anambio utafikiri Hussein bolt!! Kanikamata kafura kunipiga hata hajanipiga wala nini moja kwa moja mpk bafuni ati nifue mashuka! Ndo kwanza nilikuwa natabasam maana kufua nilikuwa sijui wkt huo njemba nyengine zipo mlangoni zinashangaa tu akaja bi maza zote zikapisha akaingia akafua[emoji23][emoji23] na kojo liliendelea kama kawa haswa ninywe ile mi juisi kola ulikuwa unanukia mkojo wa kishenzi ule! Halafu hata waniwekee makaratisi ati kojo lisifike kwenye godoro wapi kojo lile lilikuwa na ufahamu litapata upenyo tu[emoji23][emoji23]

Uziwanda una tabu zake na raha zake
Bila shaka utakuwa mkojoaji mzuri sasa hivi maana mafunzo ulishayapitia kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongereni ma last born wote kwa kutokula misoto mikali as ma first born tuliyoila .. Wengi wenu ma last born mmezaliwa wakati majumbani kwenu kumeanza kua na neema.

*Last born wetu ni wa kiume wakati mdogo mzee alikataza wadogo zangu wa kike na dada wa kazi kumsafisha akiachia vitu (k!mb@) nikapewa mimi hicho kitengo.. Aiseh ilikua balaa maana nilikua na jikoki ni kama najikinga na corona, pua na mdomo naziba na nguo, mkononi navaa softi, I was just a boy pia nilikua na kinyaa ingawa dogo nae alikua anashusha vitu vyenye tbs.. Nashukuru Mungu amekua mkubwa na anataka awe pilot.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dadek ulimchambisha alaf baadae anakuletea dharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wengine wanasomeshwaga na huku wazazi wapo... Yaani hutu tubwana mdogo tuna shida sana... halafu kwa kulalamika sasa..!!! tunaongoza kulalama hadi kero...

Unfortunately hayo madeko wengine huingia nayo hadi kwenye ndoa... Sasa ukute first born kaowana na last born ..weeeeee..... yaani huyu first born anakuwa si mwanandoa, bali mzazi wa mwenzie... Yaani katoka kulea wadogo zake na sasa analea mwanandoa kama mdogo wake
Dadek nqchagua kulea mwanandoa wangu hao wengine wakatafute mafirst born huko na wao walelewe shwain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry, hivi mnaongelea wale ambao bado mnaishi kwa wazazi ??, kwa sababu mkishaanza kujitegemea ulastborn wako utamfanyia nani ?.
 
Back
Top Bottom