Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Hollyman

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
283
Reaction score
77
Naanza kwa kuulza:
1. Naomba nipate picha halisi yaa sakata la Okwi

2.Hatua gani zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Katibu Mkuu wa Yanga aliye ishutumu vikali Kamat ya maadili, (kwan, Ulaya shutuma za hivi watu huchukuliwa hatua). Hapa sheria ipoje?

3.Unalionaje swala la kuishauri Serikali kujenga shule, mfano wa Makongo kila Kanda?
 
Mimi namuuliza analeta lini ku host kombe la Africa hapa Tanzania?
 
Hollyman na maundumla:

1.La okwi tuvute subira FIFA watoe mwongozo,woga wetu ilikuwa ni kuruhusu Yanga wachezeshe mchezaji ambaye pengine angeonekana hana uhalali.

2.TFF tulitoa onyo kuhusu matamshi ya dhihaka/uchochezi.Tunafuatilia tupate mkanda wa matamshi hayo ndipo tuchukue hatua.

3.Kupewa uenyeji AFCON bila kuandaa fainali za vijana kwanza sio rahisi.Rwanda walianza na under17 sasa 2016 wamepewa CHAN,inakwenda kwa hatua ili nchi ipate uzoefu.Sisi tumeomba fainali za vijana U17 mwaka 2019.

4.Makongo na Jitegemee ni miradi ya jeshi tunawashukuru.Tupo mbioni kuorodhesja academies zote na sports centres tujue ziko wapi,zinafanya nini,zinahitaji nini ili tijue tunaIratibu na kuziendeleza vipi ikiwa ni pamoja na ku harmonize mtaala.
 
Last edited by a moderator:
Mimi swali langu ni vipi unaichukulia kamati yako ya ligi kwa kutoa maamuzi mabovu ya mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya stand ya shinyanga na kanembo fc ya kigoma. Kwanin mechi iludiwe wakati upande mmoja haukuhusika na vurugu.
 
Hilo suala ninalifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha fairplay,kuna maagizo nimeyatoa leo mchana stand utd na kanwmbwa watafahamishwa punde.
 
Ili mpira ukue tunahitaji kuwekeza katika vijana wadogo je mmechukua hatua gani kwa soka la vijana mfano kuanzisha academy
 
Vipi kuhusu hizi timu za jeshi ambazo mmiliki wake ni mmoja, je zitapunguzwa lini na kubaki 1 kama maagizo ya Fifa yanavotaka?
 
Msisitizo wangu ni kuimarisha soma la vijana inabidi mweke sheria kali kuhakikisha Klan zinajikita kwny kuimarisha soma la vijana
 
Ili mpira ukue tunahitaji kuwekeza katika vijana wadogo je mmechukua hatua gani kwa soka la vijana mfano kuanzisha academy

Mpira wa vijana ndio mkombozi wa mpira wa Tanzania.Pamoja na jitihada zet wenyewe inabidi tujifunze kwa wenzetu hasa academies za Ivory coast (tayari tuna mawasiliano) na za Afrka kusini hasa capetown. Za hapa nyumbani tayari tumeana mawasiliano ya karibu.Uratibu ndio muhimu ili academies zetu zifanye kazi kwa pamoja,tunalifanyia kazi kwa bidii.
 
Vipi kuhusu hizi timu za jeshi ambazo mmiliki wake ni mmoja, je zitapunguzwa lini na kubaki 1 kama maagizo ya Fifa yanavotaka?

Kanuni za CAF/FIFA zinakataza mmiliki mmoja kuwa na vilabu viwili au zaidi.Kwa Tanzania inabidi tuangalie historia ya usajili wa vilabu vyetu ndipo tujue nani anamiliki klabu ipi.
 
Bishanga hata chit chat katukimbia jamani.
 
Last edited by a moderator:
Msisitizo wangu ni kuimarisha soma la vijana inabidi mweke sheria kali kuhakikisha Klan zinajikita kwny kuimarisha soma la vijana

Katika hili tuwe realistic, klabu ya ligi kuu anbayo hata kusafirisha senior team itoke mwanza iende mbeya inakuwa shida kisha uiambie isafiri na timu yao ya vijana ukweli haiyumkiniki.Tukae chini kwa pamoja tutafute wazo mbadala la ni kwa jinsi gani timu B zitacheza ligi.
 
Mh Malinzi kwanza nikupongeze kwa kuchaguliwa kwako ingawa figisufigusu zilitawala..Swali langu TFF ina mpango gani kamati ya ufundi ya team ya Taifa ambayo inaonekana inasuasua sana na kocha kama uwezo wake umefika mwisho? Pili kuna fitina zimeenea sana mtaani kuwa katibu mkuu wa TFF hakuwa na sifa za kutosha ukilinganisha na wengine walioomba. Na usaili ulifanyika na TFF yenyewe au kampuni kama tulivyozea za kpmg ! Nashukuru Mh Rais
 
Jamali Malinzi nina ushauri kwako, nakuomba mtoe ushauri kwa kila rais wa taifa letu awe anajenga uwanja/viwanja wa kisasa mfano wa Uwanja wa Taifa kila mkoa, after miaka kadhaa nchi nzima itakuwa na viwanja bora kabisa.

Anza na Kikwete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…