Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Naanza Kwa Kuulza 1. Naomba Npate Pcha Halis Ya Sakata La Okwi 2.Hatua Gan Znapaswa Kuchukuliwa Dhid Ya Katb Mkuu Wa Yanga Aliye Ishutumu Vkali Kamat Ya Maadl,{kwan Ulaya Shu2ma Za Hv Watu Huchukuliwa Hatua} Hapa Sheria Ipoje? 3.Unalionaje La Kuishaul Serkal La Kujenga Shule Mfan Wa Makongo Kila Kanda?

Andika lugha fasihi, abbreviations zako zinainyima hadhi story yako!
 
Mbna TFF km imelala iv

sio km wkt wa Tenga? Tukiacha mapungufu yake machache
 
Hollyman na maundumla:
1.La okwi tuvute subira FIFA watoe mwongozo,woga wetu ilikuwa ni kuruhusu Yanga wachezeshe mchezaji ambaye pengine angeonekana hana uhalali.
2.TFF tulitoa onyo kuhusu matamshi ya dhihaka/uchochezi.Tunafuatilia tupate mkanda wa matamshi hayo ndipo tuchukue hatua.
3.Kupewa uenyeji AFCON bila kuandaa fainali za vijana kwanza sio rahisi.Rwanda walianza na under17 sasa 2016 wamepewa CHAN,inakwenda kwa hatua ili nchi ipate uzoefu.Sisi tumeomba fainali za vijana U17 mwaka 2019.
4.Makongo na Jitegemee ni miradi ya jeshi tunawashukuru.Tupo mbioni kuorodhesja academies zote na sports centres tujue ziko wapi,zinafanya nini,zinahitaji nini ili tijue tunaIratibu na kuziendeleza vipi ikiwa ni pamoja na ku harmonize mtaala.

Jamal Malinzi kuna huyu Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Star Tv David Azaria mara nyingi nimeshuhudia vipindi vyake vingi akiwa na mtangazaji mwenzake Hilary Riami amekuwa akiisifu sana tff yako pamoja na mikakati unayoendelea nayo,vipi unamfahamu?!,na je huwa unamtuma kukufagilia namna ile ingawa asilimia kubwa ya vitu anavyozungumza ni vya kimpira na pointi zaidi?!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Umeulizwa na Crashwise kuhusu UKABILA , twasubiri majibu.

Otherwise welcome BACK to JF, vipi utarudi kule kwa kina lara 1 na Madame B? Au ndio tayari uheshmiwa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Jamal Malinzi kwanza hongera kwa ushindi ambao Jf tunajivunia member mwenzetu kuwa kiongozi wa Taasisi kubwa nchi hii ya TFF.

Pamoja na pongezi napenda kuuliza swali ambalo pengine limeshaulizwa na wenzangu, kwamba Tanzania bado tupo kwenye soka la ridhaa, lakini timu zetu yaani kuanzia vilabu mpaka timu ya taifa wanaajiri makocha (siyo consultants au wakufunzi) kutoka nchi ambazo wanacheza soka la kulipwa..... sasa ni lini unadhani Tanzania tukaingia kwenye soka la ushindani? Lini tutaondokana na Soka la ridhaa?

Pili, tumeshuhidia vilabu vikinunua wachezaji wa nje kwa gharama kubwa, na kuwalipa fedha nyingi kulinganisha na wachezaji wa ndani, sasa hauoni kwamba kwakuwa nchi yetu ipo kwenye soka la ridhaa jambo hili linaweza kuwashusha morale wachezaji wa ndani wanaojituma kuliko hao wa nje wenye majina tu? Na nini matarajio yako kuhakikisha wachezaji wetu wa ndani wanaojituma wanathaminiwa sawa na wanaotoka nje?
 
Last edited by a moderator:
Mh rais wa TFF,

Hili tatizo la vijana wa kitanzania wanapopata bahati ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya na kisha kususi, mfano Haruna Moshi na Shomar Kapombe, nyinyi kama tff mme/mnalishughulikiaje ili angalau nchi yetu iwe na akina Samatta na Ulimwengu wengi??
 
Mh Malinzi kwanza nikupongeze kwa kuchaguliwa kwako ingawa figisufigusu zilitawala..Swali langu TFF ina mpango gani kamati ya ufundi ya team ya Taifa ambayo inaonekana inasuasua sana na kocha kama uwezo wake umefika mwisho? Pili kuna fitina zimeenea sana mtaani kuwa katibu mkuu wa TFF hakuwa na sifa za kutosha ukilinganisha na wengine walioomba. Na usaili ulifanyika na TFF yenyewe au kampuni kama tulivyozea za kpmg ! Nashukuru Mh Rais

Stay tuned kuhusu technical department.
la ajira mjadala ushafungwa,tunasonga mbele kuelekea kuboresha mpira wetu.
 
Jamali Malinzi nina ushauri kwako, nakuomba mtoe ushauri kwa kila rais wa taifa letu awe anajenga uwanja/viwanja wa kisasa mfano wa Uwanja wa Taifa kila mkoa, after miaka kadhaa nchi nzima itakuwa na viwanja bora kabisa.

Anza na Kikwete.

Ahsante Arushaone, lakini kabla ya kujenga viwanja vipya hebu kwanA tuboreshe vilivyopo.TFF ina uwezo wa kupata wabia wa kuendeleA viwanja vyetu muhimu iwepo will kwa wamiliki.
 
Last edited by a moderator:
Stay tuned kuhusu technical department.
la ajira mjadala ushafungwa,tunasonga mbele kuelekea kuboresha mpira wetu.

Kuna mpango wa kuwezesha makocha wazawa nao kuchukua team ya taifa? Maana nchi kama Nigeria mzawa anafanya vizuri sana na hii inaamsha molari ya wachezaji sana..
 
Jamal Malinzi kuna huyu Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Star Tv David Azaria mara nyingi nimeshuhudia vipindi vyake vingi akiwa na mtangazaji mwenzake Hilary Riami amekuwa akiisifu sana tff yako pamoja na mikakati unayoendelea nayo,vipi unamfahamu?!,na je huwa unamtuma kukufagilia namna ile ingawa asilimia kubwa ya vitu anavyozungumza ni vya kimpira na pointi zaidi?!

nikujibuje ndugu yangu?
 
Mkuu Jamal Malinzi kwanza hongera kwa ushindi ambao Jf tunajivunia member mwenzetu kuwa kiongozi wa Taasisi kubwa nchi hii ya TFF.

Pamoja na pongezi napenda kuuliza swali ambalo pengine limeshaulizwa na wenzangu, kwamba Tanzania bado tupo kwenye soka la ridhaa, lakini timu zetu yaani kuanzia vilabu mpaka timu ya taifa wanaajiri makocha (siyo consultants au wakufunzi) kutoka nchi ambazo wanacheza soka la kulipwa..... sasa ni lini unadhani Tanzania tukaingia kwenye soka la ushindani? Lini tutaondokana na Soka la ridhaa?

Pili, tumeshuhidia vilabu vikinunua wachezaji wa nje kwa gharama kubwa, na kuwalipa fedha nyingi kulinganisha na wachezaji wa ndani, sasa hauoni kwamba kwakuwa nchi yetu ipo kwenye soka la ridhaa jambo hili linaweza kuwashusha morale wachezaji wa ndani wanaojituma kuliko hao wa nje wenye majina tu? Na nini matarajio yako kuhakikisha wachezaji wetu wa ndani wanaojituma wanathaminiwa sawa na wanaotoka nje?
Nianze na la foreign players, ukweli ni kwamba uwekezaji kwa program za vijana ni mdogo ndio maana tuna import vipaji,inabidi tuwekeze kwa vijana.
La walimu wa nje hatuna njia, nchi yetu ina makocha registerd 2000 na mia tano wako dar,shule za msingi Iko elfu kumi na sita achilia mbali sekondari,jiulize tunapate walimu wa kufundisha mpira nchi hii ngazi ya vijana? Ni mtihani,bila youth football ni vigumu kupata timu za taifa nzuri.
La kutoka amateur kwenda full professionalism lina ugumu wake tokana na muundo wa umiliki wa vilabu vyetu,tuna vilabu vya kijamii (yanga,simba,coastal etc), vya kampuni binafsi (mtibwa,azam,KSugar) na vya serikali (polisi,jkt ruvu,prisons).Ukitaka full professnalism lazima ukubali free transfer of players,je tuko tayari kwa hilo? As it stands we are semi pro.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mpango wa kuwezesha makocha wazawa nao kuchukua team ya taifa? Maana nchi kama Nigeria mzawa anafanya vizuri sana na hii inaamsha molari ya wachezaji sana..

Nakubaliana na wewe,walimu wetu inabidi waanze na vijana wawakuze wakiwa nao kama wanavyofanya wenzetu.
 
Jamal Malinzi mimi nitarudi hapa kesho nikutwange maswali kadhaa ambayo mengi yataegemea kwenye ufundi zaidi...

Kwa sasa ngoja niegeshe mbavu zangu naamini uzi huu utakuwa endelevu...
 
Last edited by a moderator:
Mh rais wa TFF,

Hili tatizo la vijana wa kitanzania wanapopata bahati ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya na kisha kususi, mfano Haruna Moshi na Shomar Kapombe, nyinyi kama tff mme/mnalishughulikiaje ili angalau nchi yetu iwe na akina Samatta na Ulimwengu wengi??

Ishu hapa ni professionalism. Je kisaikolojia tunawaandae vijana wetu kucheza nje? Zinedine Zidane alianzia AS Cannes akawa superstar,Kapombe kapata hiyo fursa ataitumiaje?
 
Jamal Malinzi mimi nitarudi hapa kesho nikutwange maswali kadhaa ambayo mengi yataegemea kwenye ufundi zaidi...

Kwa sasa ngoja niegeshe mbavu zangu naamini uzi huu utakuwa endelevu...

Unakimbia PM? Ngoja mods wa pm Mentor nimshtue
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom