Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

kwanini kamati ya hadhi na sheria inabariki uvunjwaji wa katiba za wanachama wake hamuoni hali hii inaweza kuwafanya wadau wakapoteza imani na kuamua kufungua kesi mahakamani mfano wakati wa sakata la simba kati ya kamati ya utendaji na mwenyekiti wake ilionekana wazi katiba ilivunjwa kutokana na kushindwa kujazwa nafasi ya makamu ya uenyekiti baada ya siku 90 lakini bado wameendelea kukaid maagizo ya tff ya kutoitisha uchaguzi hamuoni mnakaribisha mgogoro mwingine
 
Mkuu Jamal Malinzi habari za asubuhi?!

Ukishaamka na kuingia humu tujulishe ili tuendeleze pale tulipoishia jana,kwa sbb tunapenda kujua zaidi mambo mengi sana kuhusu TFF!!.
 
Last edited by a moderator:
kwanini kamati ya hadhi na sheria inabariki uvunjwaji wa katiba za wanachama wake hamuoni hali hii inaweza kuwafanya wadau wakapoteza imani na kuamua kufungua kesi mahakamani mfano wakati wa sakata la simba kati ya kamati ya utendaji na mwenyekiti wake ilionekana wazi katiba ilivunjwa kutokana na kushindwa kujazwa nafasi ya makamu ya uenyekiti baada ya siku 90 lakini bado wameendelea kukaid maagizo ya tff ya kutoitisha uchaguzi hamuoni mnakaribisha mgogoro mwingine
Kamati ya utendaji ya Simba tayari imekaa na kutoa mwelekeo.TFF si nia yetu kuingilia masuala ya wanachama wetu,tunafanya hapo tu ikibidi.
 
Lini mtaanza kutoa electronic tickets with seat numbers for every match pale uwanja mpya?
 
kunafununu kwamba TFF imejaa watu wa kabila lako, hii ikiwa ni baada ya wewe kuingia. Ufafanuzi tafadhali
 
Bw. Jamal Malinzi nimerudi tena, nitakuwa nauliza swali moja moja ili uweze kutujibu kwa kina kidogo.

Kwa nchi zilizoendelea kisoka kama Brazil, Ujerumani, Uholanzi n.k huwa zina mfumo wa uchezaji wa kabumbu (falsafa ya uchezaji).

Kwa namna fulani mifumo hii tunaweza kuiita ni tamaduni zao za kisoka ambapo kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ya taifa, wachezaji na timu za vilabu zina exercise utamaduni huu...

1. Je, sisi Tanzania tuna mfumo wowote wa kisoka hadi sasa?

2. Na kama hatuna, je kuna mipango gani ya kujaribu kutengeneza mfumo au utamaduni wa kisoka utaokuwa ni wa kitanzania na wenye tija?

3. Leodgar Tenga alijaribu kuishi katika falsafa ya mpira wa Kidenishi, je huu ndio mfumo ambao tumeamua kuunakili?
 
Last edited by a moderator:
Lini mtaanza kutoa electronic tickets with seat numbers for every match pale uwanja mpya?

Electronic ticketing tumeanza ila kwa kweli kwa yaliyotokea leo mkwakwani Tanga itabidi kesho tuchukue hatua za dharura kulinda usalama wa watazamaji wa mpira.Taarifa nilizoletewa leo kutoka Tanga si nzuri.
 
Bw. Jamal Malinzi nimerudi tena, nitakuwa nauliza swali moja moja ili uweze kutujibu kwa kina kidogo.

Kwa nchi zilizoendelea kisoka kama Brazil, Ujerumani, Uholanzi n.k huwa zina mfumo wa uchezaji wa kabumbu (falsafa ya uchezaji).

Kwa namna fulani mifumo hii tunaweza kuiita ni tamaduni zao za kisoka ambapo kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ya taifa, wachezaji na timu za vilabu zina exercise utamaduni huu...

1. Je, sisi Tanzania tuna mfumo wowote wa kisoka hadi sasa?

2. Na kama hatuna, je kuna mipango gani ya kujaribu kutengeneza mfumo au utamaduni wa kisoka utaokuwa ni wa kitanzania na wenye tija?

3. Leodgar Tenga alijaribu kuishi katika falsafa ya mpira wa Kidenishi, je huu ndio mfumo ambao tumeamua kuunakili?

Ahsante watu8.Kuna nchi (si zote) zimebuni falsafa ya uchezaji wa mpira nchini mwao,mifano mizuri ni spain,ujerumani na italy,waingereza ndo wanakukuruka kutafuta mfumo thabiti hawajaupata.Youth development plan tunayoiandaa inatutaka tutengeneze Football curicullum (mtaala),ikiwa tayari itatoa mwongozo kwa shule zote za mpira nchini.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nna maswali kidogo ukinijibu ntashukuru

siku hizi huwa tunasikia timu za bongo hapa
mfano African Lyon na Moro united zinauzwa

mara unasikia hii imeuzwa na hii imehamishwa

je utaratibu uko vipi?

nyinyi TFF mnahusikaje?

bei ya timu zilizowahi kuuzwa hadi sasa ilifika milioni ngapi?

je kuna timu zipo sokoni?

Moro United imeishia wapi??????
 
Sincerely speaking we need time kuruhusu electronic ticketing uwanja wa taifa.Hebu tusubiri tuone nini kinaendelea kwenye viwanja vyenye watazamaji wachache.

Mh, kwa nini tusubiri pale Uwanja wa Taifa? Ni kitu gani kigumu? Hoja kwamba tuanze viwanja vyenye mashabiki wachache kwanza inaleta maswali mengi na ukakasi mwingi
Tufafanulie katika hili
 
CHAZA nashukuru tulichukua tahadhari kwa kuanza na mechi zenye small crowds.Yaliyotokea leo mkwakwani Tanga ingekuwa uwanja wa taifa yanga vs simba ingekuwa maafa.Inabidi tujipange vizuri zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nna maswali kidogo ukinijibu ntashukuru

siku hizi huwa tunasikia timu za bongo hapa
mfano African Lyon na Moro united zinauzwa

mara unasikia hii imeuzwa na hii imehamishwa

je utaratibu uko vipi?

nyinyi TFF mnahusikaje?

bei ya timu zilizowahi kuuzwa hadi sasa ilifika milioni ngapi?

je kuna timu zipo sokoni?

Moro United imeishia wapi??????

The Boss,Tanzania tuna vilabu vya aina tatu,community owned (yanga,simba,coastal etc),vya kampuni binafsi (azam,mtibwa,KSugar,africa lyon etc) na vya serikali (prisons,jkt's na polisi).Vya serikali haviuziki,vilivyobaki vinauzika kwa ridhaa ya wamiliki.TFF inachokataza ni The Boss kununua malinzi fc ya masasi kisha ukataka eti unahiamishia Dar,ukinunua timu inabaki kuchezea pale ulipoikuta.Bei maelewano.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi unajulikana sana kama wewe ni kada wa timu ya Yanga unatuhakikishia nini sisi wana msimbazi je utaweza kuwa fair especially inapotokea utata ambao wewe unatakiwa usolve maana tunaona kwenye hata ishu ya okwi kama umelalia upande wa yanga
 
asante
kwa majibu
naomba unijibu kuhusu ilipo Moro United
 
Ahsante watu8.Kuna nchi (si zote) zimebuni falsafa ya uchezaji wa mpira nchini mwao,mifano mizuri ni spain,ujerumani na italy,waingereza ndo wanakukuruka kutafuta mfumo thabiti hawajaupata.Youth development plan tunayoiandaa inatutaka tutengeneze Football curicullum (mtaala),ikiwa tayari itatoa mwongozo kwa shule zote za mpira nchini.

Okay,

Nadhani haya uliyofafanua hapa ya mtaala wa michezo ni kama alivyopata kufafanua Bw. Mweisigwa akihojiwa na TBC kama sikosei mwezi uliopita...

Lakini najiuliza huu ni mpango wenu TFF au kuna msaada toka serikalini?

Kuna wakufunzi wa kutosha au kwa kuanzia kuna shule kadhaa zitahusika? (Nakumbuka ziara uliyoifanya Alliance Academy na ahadi uliyotoa ya kuiingiza shule ile katika mpango kama huu ulioeleza hapa).
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi unajulikana sana kama wewe ni kada wa timu ya Yanga unatuhakikishia nini sisi wana msimbazi je utaweza kuwa fair especially inapotokea utata ambao wewe unatakiwa usolve maana tunaona kwenye hata ishu ya okwi kama umelalia upande wa yanga

Si kweli,maana hata Yanga wanalalamika.Kikubwa katika suala la Okwi TFF tumechukua tahadhari ili vilabu vyetu visiingie matatani na FIFA.Sipendelei upande,trust me katika hilo.Uzuri siasa za yanga/simba nilijifunzia katika tanuru la ukatibu mkuu wa Yanga.
 
Back
Top Bottom