Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

Upatikanaji wa tickets za world cup kule Brazil kupitia TFF kwa watanzania huu ukoje? Ni taratibu gani inabidi nifuate ili niweze kupata tickets ambazo TFF imekuwa-allocated na FIFA?
Wahi kutuma maombi kupitia tanfootball@tff.or.tz deadline ni tarehe 07 february.
 
Sasa kama TFF hampati chochote kwenye makato ya mapato ya mechi za ligi kuu, mnajiendeshaje, Mnaendeshaje Ligi na nini chanzo cha mapato yenu?
 
Mie nna maswali mawili tu ningependa kupata ufafanuzi...la kwanza ni nidhami kwa wachezaji.najua ni jukumu la club kuangalia nidhamu ya wachezaji wake lakini nyinyi kama tff mnafanya nini walau kuleta adabu katika soka la bongo?baadhi ya wachezaji wameonekana kwenye mikanda ya utupu na mapicha yasiofaa kuonekana ktk jamaa.. wangine wanaonekana wakivuta bangi na membo mengin mengi yasiofaa kwa jamii na kwa bahati mbaya si tff wala club zao wanaojitokeza na kukemea mambo yale.la pili ni kuhusu wachezaj wa kigeni..wachezaji wa kigeni ingefaa wawe ni wachezaji wa timu zao za taifa hii ingeleta changamoto kwa wachezaji wetu wa ndani,sio mchezaji anasafiri zaidi ya mail 5,000 anakuja kukaa benchi.
 
Kwanza nikupongeze sana Swahiba Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa raisi wa Shirikisho La Mpira wa Miguu Tanzania. Mimi nigependa kufahamu juhudi za TFF kuboresha hivi vyama vya soka mikoani. Ki uhalisia vyama hivi vimekuwa na juhudi finyu sana katika kuendeleza soka. Ni mara chache sana vyama hivyo vimekuwa havina juhudi za kuendesha ligi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa katika mikoa mbalimbali. Je TFF ina juhudi gani kuhakiki kuwa vyama hivyo vinasimamia uendelezaje wa soka katika mikoa yao?
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe suala la mgao ni tatizo.Kwanza katika hiyo asilimia 52% inayokatwa Serikali inachukua VAT 18%.TFF royalty inayopata (mrahaba) ni sifuri 0% hiyo FDF kwa mujibu wa sheria ni kwa ajili ya miradi ya vijana,maana yake ligi yetu haichangii TFF hata hela ya kununua LUKU.Yote haya yanajadilika ili tutafute formula nzuri ya kumsaidia kila mhusika vikiwemo vilabu.
Nashukuru kwa mwitikio wako, suala la VAT ni gumu kwa sababu lipo kisheria ndo maana katika pendekezo langu la baadhi ya wadau kupunguziwa mgawo suala la VAT na TFF sikuweka.

Swali lingine, mara nyingi TFF mmekuwa mkitoa mkitangaza mapato pamoja na mgawanyo wake kwenye mechi zinazohusisha Simba na Yanga pamoja na timu za Taifa na hasa mechi zake zinapofanyika uwanja wa Taifa, kwa nini hatusikii mkitangaza mapato ya mechi zingine?, mfano ya Coastal Union dhidi ya JKT Oljoro, Kagera Sugar dhidi ya Mbeya City na hata ile Azam dhidi ya Mtibwa.
 
Sasa kama TFF hampati chochote kwenye makato ya mapato ya mechi za ligi kuu, mnajiendeshaje, Mnaendeshaje Ligi na nini chanzo cha mapato yenu?
Tupo kwenye mchakato wa kiangalia upya muundo wa makato.In the meantime tuna survive kwa vyanzo mbadala kama mechi za timu za taifa,asilimia ya mgao wa azam na vodacom n.k Its very hard hasa kuendesha timu za vijana na za wanawake,ndio maana tunataka tujenge investment house pale karume ilala.
 
Mie nna maswali mawili tu ningependa kupata ufafanuzi...la kwanza ni nidhami kwa wachezaji.najua ni jukumu la club kuangalia nidhamu ya wachezaji wake lakini nyinyi kama tff mnafanya nini walau kuleta adabu katika soka la bongo?baadhi ya wachezaji wameonekana kwenye mikanda ya utupu na mapicha yasiofaa kuonekana ktk jamaa.. wangine wanaonekana wakivuta bangi na membo mengin mengi yasiofaa kwa jamii na kwa bahati mbaya si tff wala club zao wanaojitokeza na kukemea mambo yale.la pili ni kuhusu wachezaj wa kigeni..wachezaji wa kigeni ingefaa wawe ni wachezaji wa timu zao za taifa hii ingeleta changamoto kwa wachezaji wetu wa ndani,sio mchezaji anasafiri zaidi ya mail 5,000 anakuja kukaa benchi.

1.Kanuni za maadili za TFF (ethics code) zinawabana na wachezaji maana nao ni TFF family.Ndugu kama una ushahidi wa madudu uliyoyasema nitumie jamalmalinzi@yahoo.com au nipigie 0754815543.
2.Ni kweli lazima tuweke vigezo vya kusajili foreign players kama ilivyo kwa wenzetu,ngoja tulifanyie kazi.
 
Kwanza nikupongeze sana Swahiba Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa raisi wa Shirikisho La Mpira wa Miguu Tanzania. Mimi nigependa kufahamu juhudi za TFF kuboresha hivi vyama vya soka mikoani. Ki uhalisia vyama hivi vimekuwa na juhudi finyu sana katika kuendeleza soka. Ni mara chache sana vyama hivyo vimekuwa havina juhudi za kuendesha ligi mbalimbali kuanzia ngazi za chini kabisa katika mikoa mbalimbali. Je TFF ina juhudi gani kuhakiki kuwa vyama hivyo vinasimamia uendelezaje wa soka katika mikoa yao?

Katiba ya FAT ilivinyima vyama vya mikoa uhuru wa kuamua mambo yao wenyewe,katiba ya shirikisho inavipa vyama vya mikoa uhuru mpana sana wa maamuzi,ni juu ya vyama kutumia fursaa hii na kuwa wabunifu.Tatizo la pesa ni kubwa sana na vingi vinashindwa kuanzisha mashindano yao au miradi yao,ni vyema vikashirikiana hata kama ni ngazi ya kanda kuanzisha mashindano yao.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ningependa kujua katika kanuni,sheria na taratibu zenu za kiutendaji!!neno BUSARA ni sahihi kutumika katika ukiukwaji wa sheria??maana katika miaka michache iliyopita,tumesikia neno hlo likitumika mara nyingi katika kupindisha sheria na kanuni zenu mlizojiwekea

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kiongozi mchakato wa kuipigania ZANZIBAR FIFA NA CAF UNAENDELEAJE, tukiwa na kalata mbili itatusaidia sanaa!
 
Fufua kombe la taifa na uongeze timu za ligi kuu kuwa 18-20 na ligi isisimame miezi mitatu.......
 
Hadi mwisho hakuna Jamal Malinzi alipogusia suala la ukabila. kumbe inawezekana ni kweli siyo? kwa nini husitoe ufafanuzi
 
Last edited by a moderator:
Unazungumziaje suala la ukabila ndani ya TFF, hili swali kuna wadau wameuliza lakini nakushangaa haujibu!!!
 
Malinzi nakushangaa sana unaposema kuwa mnajiandaa kutengeneza soka la wanawake Tz, majuzi tu nimepata habari kutoka kwa Mchezaji wa Twiga Starz akidai maandalizi ni mabavu sana na nilisikitika kuniambia hata kocha wa makipa hakuwepo bado, ni vema ukatujibu ukweli kulilo kutupa majibu ya kutufariji. Maandalizi kwa Team ya Taifa ya Wanawake ni mabovu, ongea na wachezaji wenyewe wakwambie.
 
Hadi mwisho hakuna Jamal Malinzi alipogusia suala la ukabila. kumbe inawezekana ni kweli siyo? kwa nini husitoe ufafanuzi

hili jambo lipo Mkuu, na kuonesha kuwa hata yeye amelifurahia tunamuuliza maswali ktk hili ili atoe ufafanuzi yeye ananyamaza kimya, inawezekana bado tuna viongozi mizigo.
 
Last edited by a moderator:
Ni vizuri sana kuonge na wapenda michezo wa tanzania, ila nakuomba yale wanayo shauri uwe unayapima na mengine kuyafanyia kazi,Naomba ligi kuu iwe na timu 20, ligi daraja la kwanza, la pili, tatu na nne zichenzwe kama ilivyo ligi kuu, kusiwe na vituo, itasaidia kupata wachezaji wazuri wa timu ya taifa na ligi kuu nzuri, sababu mchezaji atakae cheza ligi kuu atakuwa kapitia tabu zote la ligi ndogo tofauti na sasamchezaji ligi kuu anafundishwa jinsi ya kupiga pasi ni aibu1) Wachezaji hawajui nidhamu ya mpira2) Hawajitambui3) Mchezaji hana wakala4) mchezaji wa ligi kuu anacheza ndondo,Yote hayo yanasababishwa na kutokujitambua kwa wachezaji, lakini kama akipitia ligi zote hizo itakuwa inasaidia kupata elimu kidogo
 
hili jambo lipo Mkuu, na kuonesha kuwa hata yeye amelifurahia tunamuuliza maswali ktk hili ili atoe ufafanuzi yeye ananyamaza kimya, inawezekana bado tuna viongozi mizigo.
Kama umetumwa na nyamlani mwambie hawapo..mpira sio siasa uwezi kumuita mtu mzigo wakati hana hata miez mitatu offisin..otherwise wwe ndo mzigo wa kufikili..hvi nyie wachangga mnamatatizo gani.?.mnalazimisha kuchaguliwa wakati uko kwnu akuna timu hata ya daraja la nne.
 
Back
Top Bottom