Uzi wa tafiti na Saikolojia

Uzi wa tafiti na Saikolojia

Njaa husababisha kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini. Ili kujilinda na kufanya utendaji uendelee kama kawaida, mwili huzalisha homoni mbili ambazo ni 'Adrenaline na Cortisol'.

Homoni hizo husaidia kuongeza kiwango cha sukari lakini pia huuweka mwili kwenye tahadhari ya kupambana na kitu chochote, na hapo ndipo hasira huwa ni rahisi kutokea!
#Tafiti
 
Spotify: Ilianzishwa rasmi mwaka 2006, lakini ilianza kuzalisha rasmi faida kuanzia mwaka 2019.

Spotify ni moja ya mtandao maarufu wa kusikiliza muziki, una watumiaji hai milioni 626 na wanaolipia ni milioni 246.
#Tafiti
 
Ndoto za kutisha na majinamizi hutokea ili kumuamsha usingizi kutokana na akili imegundua kuna shida kama tukiuacha mwili uendelee kulala hivyohivyo.

Kiufupi ndoto ya kutisha hufanya kazi kama sindano ya adrenalini kumzindua anayelala asije pitiliza akakufa.

Kwa waamini: kazi ya malaika mlinzi na sio 'shetani' badala ya kukemea tunapaswa kushukuru kwa kuamshwa haraka tukaishi.
#Utafiti
 
👏👏👏🙏
Shukrani sana kwa kujazia maelezo mkuu
 
Malimao husaidia kupooza homa inayotokana na malaria, matokeo yake mtu anabaki kuwa na kuugua 'kichinichini' kwa muda mrefu malaria hiyo hivyo anapungukiwa damu.

Kinachopunguza damu ni malaria na sio malimao. Tenaa kiukweli kutokana na kuwa na vitamin C kwa wingi malimao yanasaidia kuongeza damu kwa kuongeza ufanisi wa ufyonzaji wa madini chuma katika chakula ambayo ni muhimu kwa kuongeza damu.

Malaria na kukausha damu ni matokeo ya uhusianisho na sio usababishano. Mbaya wa kweli hapo ni hiyo, malaria iliyofichwa homa.
#Utafiti
 
Binadamu akiamka ni mwepesi kukumbuka upande alioamkia, mfano: ubavu wa kushoto, ubavu wa kulia, au mgongo na/ tumbo.

Lakini binadamu huyo huyo hawezi kukumbuka upande ambao usingizi ulimpata. Yaani hawezi kukumbuka kama wakati usingizi umempata alilalia ubavu wa kushoto/ kulia au tumbo na/ mgongo.
 
Back
Top Bottom