Uzi wa ushahidi wa mambo ya kusikitisha katika uchaguzi mkuu wa 2020

Uzi wa ushahidi wa mambo ya kusikitisha katika uchaguzi mkuu wa 2020

Mikoani huko kamatakamata inatisha. Kuna wananchi weengi wamo korokoroni kwa ama kutokukubaliana au kuhoji wizi na figisu za ccm kwenye uchaguzi
Mkuu, hii ni kiujumla mno; haisaidii kitu chochote.

Tunataka ushahidi. Hawa walioko korokoroni hawana majina au hata sehemu waliko hazijulikani?
 
Aisee haya mambo ni ya aibu kubwa mno!!
 
Mkuu, hii ni kiujumla mno; haisaidii kitu chochote.

Tunataka ushahidi. Hawa walioko korokoroni hawana majina au hata sehemu waliko hazijulikani?

Kaka kule inbox umegoma kunipa mrejesho!
 
Mkuu, hii ni kiujumla mno; haisaidii kitu chochote.

Tunataka ushahidi. Hawa walioko korokoroni hawana majina au hata sehemu waliko hazijulikani?
Mkuu, Kama una uwezo wa kufanya chochote fuatilia mkoa wa Mara (hasa Tarime na Rorya), Simiyu na Singida. Utashangaa sana.

Pia, ukiacha Dar, naskia maeneo mengine mengi ni hivo hivo.

Wale unaskia wanakimbia usifikiri wanaigiza
 
Ongeza - karatasi za kura zilizobaki kwenye vituo baada ya upigaji kura, wasimamizi waliambiwa, wazipige upande wa CCM na kuingiza kwenye masanduku ya kura.
Vituo vyote vya kupigia kura Tanzania wasimamizi wakuu walielekezwa kuongeza kura kwa ccm.
 
1605256248539.png

Jamaa aliniudhi sana na kuniangusha. Tumepiga kura wote kisha akanishawishi eti nitafute wenzangu kama 100 tupige kelele na kuandamana kama hatuna akili atanipa shillingi laki mbili., kumbe alishapanga tukio akamatwe aje kusingizia anataka kuuliwa ili akaishi Ulaya.Kwa kweli Lissu wewe ni msaliti, nataka hela zangu.
 
Wana JF,

Huu uzi ni wa kumbukumbu. Weka hapa mambo yote ya kusikitisha yaliyotokea katika uchaguzi mkuu wa 2020. JF ni sehemu ya kuelimishana na kutunza kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Tafadhali weka hapa picha, video, maelezo, ama visa vya mambo mbalimbali ya kusikitisha uliyoyashuhudia ama kuyasikia ya KUSIKITISHA kuhusu uchaguzi wa 27 na 28 Oktoba 2020. Internet imerejeshwa sasa. Lete ma-video, picha, nk ambazo ulipiga lakini haukuweza kutuma kwa kukosa internet.

Kulikuwa na visa vya kusikitisha hata kabla ya uchaguzi. Wagombea wa upinzani walienguliwa kwa njia za kimafia kama kutekwa, kukamatwa na kufungwa ili muda wa kurudisha fomu upite, kunyang'anywa fomu kwa nguvu, kushawishiwa kwa pesa, nk.

NEC ina wajibu wa kuwasaidia wagombea katika kujaza fomu lakini iliwatafutia sababu ili kuwaengua. Mathalani, wakati wagombea wengine walienguliwa kwa fomu zao kuwa na jina la chama kama CHADEMA (badala ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO), wengine walienguliwa kwa kuandika CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO badala ya CHADEMA.

Wakati wagombea wengine walienguliwa kwa kujaza CHADEMA kwenye fomu kama jina la chama, NEC ilipotoa fomu ya kupigia kura, iliweka CHADEMA kama jina la chama kwenye fomu hiyo!

Wagombea waliokata rufaa, NEC ilikalia rufaa zao. Wale ambao zilisikilizwa, ilichukuwa zaidi ya mwezi kutoa uamzi! Na uamzi ulipotolewa, wale walioshinda, hawakupewa barua za kushinda rufaa. Na kwa hiyo hawakuruhusiwa kufanya kampeni. Kuna Wakati Mahera aliwaomba Wasimamizi wa Majimbo wawape barua kana kwamba hawawajibiki kwa NEC!

Kuna mgombea ambaye hakuruhusiwa kufanya kampeni baadhi ya mikoa ya kusini japo alikuwa na ratiba hiyo kutoka NEC. Alidanganywa kuwa kulikuwa na kimbunga mikoa hiyo ili asiende huko. Wahudhuriaji katika mikutano yake walipigwa mabomu ya machozi. Kampuni za simu zilizuia taarifa za kumhusu mgombea huyo kutumwa katika mitandao yao!

Wakati wa kampeni, vyombo vya habari vilitangaza habari za mgombea mmoja tu kwa kiasi kikubwa. Na kuhujumu kampeni za wagombea wengine.

Vyombo vya serikali vilihujumu baadhi wa wagombea kwa makusudi kabisa. Feri kati ya Ukerewe na Kisorya, ilikataa kumvusha hyo mgombea wa upinzani. Mamlaka ya Anga ilikataa kutoa kibali cha chombo chake kuruka.

Kuna mgombea kule Zanzibar (ACT) alifungiwa kwa siku 5 kwa kuhamasisha wapigakura wake kwenda kupiga kura tarehe 27 Okt 2020. Mgombea wa CCM pia alisikika akitoa ujumbe huo huo, tena kwenye tepu/mkanda. ACT walipolalamika, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa mgobea wa CCM.

Vyama viliruhusiwa kuunga mkono chama tawala lakini vikakatazwa kuunga mkono vyama vikuu vya upinzani! Haya yote yalifanyika chini ya sheria moja za nchi moja ya Tanzania.

NEC ambayo ni chombo cha kutoa haki kwa wagombea kilikuwa kinyume kabisa. Ghafla NEC walishindwa kujua kuwa katika Alfabeti, huwa inaaza A (ACT nk) halafu ndio herufi nyingine zinafuata. Wakaamua kuanza na C (CCM) kwenye karatasi ya kura! Na C nyingine (CHADEMA) ikawekwa mwisho kabisa mwa karatasi ya kura.

NEC na Msajili wa Vyama walitayarisha sheria/kanuni za kufanikisha kuharibu uchaguzi na kulazimisha vyama kutia sahini. Vyama ambavyo visingesaini, visingeruhusiwa kushiriki uchaguzi! Kanuni hizo ni pamoja na NEC kutokulazimika kutoa nakala ya matokeo vituoni kwa mawakala, kuwaapisha mawakala katika makao makuu ya majimbo tu, kutokuwapa mawakala barua ya utambulisho baada ya kuapa...

Sheria inayokataza Mawaziri na Rais kutoa ahadi/pesa kwa wananchi wakati wa kampeni haikuzingatiwa kabisa. Vyama vya upinzani vilipolalamika, havikusikilizwa mwanzo hadi mwisho.

Serikali ilkataa pesa kutoka washirika wa maendeleo na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uchaguzi huu. Serikali ilikwisha panga kile ambacho sisi hatukujua mpaka upigaji kura ulipofanyika. Katika mambo hayo ni kutokuwepo kwa waangalizi kutoka nchi washirika wa maendeleo na Umoja wa Mataifa.

Kuna mgombea wa Urais na mgombea mwenza walikuwa wanasema kuwa hata wasipopigiwa kura watashinda. Wale wanaopigia kura vyama vingine wanajisumbua tu. Baada ya uchaguzi ndio nikajua walikuwa wanamaanisha nini.

Mkurugenzi wa NEC alitumika kupigia chama tawala kampeni wazi wazi bila aibu! Kuna wakati alijibu hoja za wapinzani kwa niaba ya CCM (km kuhusu madini yetu). Angalau Kaijage alikuwa kimya. Mahera alishindwa kabisa kuwa kimya! ZEC ilishirikiana na CCM kufoji fomu ya kiapo ya Maalim Seif ili kumuengua. Kugushi ni kosa la jinai lakini yaliisha kimya kimya!

Baadhi ya maamzi haya yalifanywa na watu ambao wamesomea sheria na utoaji haki, majaji "waliobobea", wengine walitumikia nchi katika ngazi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Sijui hili linawaambia nini Watanzania kuhusu utoaji haki katika nchi yao. Watu wenye kesi mahakamani hapa Tanzania, je wana imani yoyote na mfumo wa utoaji haki nchi hii?

Uchaguzi 2020 - Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha.

View attachment 1625181
View attachment 1625182
Ushahidi mwepesi kwa tuhuma nzito!! Acheni propaganda za kuchafua nchi wakati mnajua kabisa masuala haya yamejaa URONGOOO na GHILIBA kubwa!

Hata Rais Trump analalamika ila Kwa ushahidi mweupe na jinsi Mahakama ilivyoukataa tusubiri tuone Rais Biden akipelekwa ICC!

Queen Esther
 
Marekani ingekuwa kama Tanzania, Trump angetumia mahakama, NEC, jeshi, polisi, Mamlaka ya Anga, makampuni ya simu, TISS, TCRA, nk kubaki madarakani. Ungekuwa na akili hata kidogo, ungejua kuwa kwa vile Marekani siyo Tanzania, Trump anaondoka.
Ushahidi mwepesi kwa tuhuma nzito!! Acheni propaganda za kuchafua nchi wakati mnajua kabisa masuala haya yamejaa URONGOOO na GHILIBA kubwa!

Hata Rais Trump analalamika ila Kwa ushahidi mweupe na jinsi Mahakama ilivyoukataa tusubiri tuone Rais Biden akipelekwa ICC!

Queen Esther
 
Ushahidi wa kusikitisha zaidi kwangu na iwe kumbukumbu ya daima kwa vizazi vijavyo ni jinsi wanaoitwa wapinzani pamoja na kujimwambafy kuchukua nchi asubuhi na mapema kuishia kupokea kipigo cha mbwa koko kutokana na sera zao mbovu ambazo wananchi wamezikataa kupitia sanduku la kura, hakika watanzania sio wajing
Kodi za wananchi waliodhulumiwa haki yao
Ni ziaid ya UCHAFUZI ,Bilioni zaidi ya 500 serikali imepoteza kwenye UTOPOLO Huu wa Tar 27 na 28 Oct 2020.
 
JamiiForums naomba msiufute uzi huu. Jana kamati ya maadili iliwatembelea, mmeongea mengi na mmekubaliana mengi. Nadhani pia mmepigwa speed limit ili mminye baadhi ya nyuzi hasa za kumkosoa Kayafa na CCM yake. Lakinj huu uzi una manufaa makubwa Sana kwa historia ya nchi yetu
Nowdays jf is not where we dare to talk openly... Tuliamini hapa n sehemu ya kutoa ya moyoni yasiyoweza kutolewa in other platforms but saivi wanayazuia!! Its real bad!
 
Ni ubabe wa kutisha...Natumia kodi yenu, mda wenu na attention yenu kwenye matokeo ya kura zenu kumbe sio zenu,anayebisha anaharibu amani anapigwa anateswa na ikibidi anauawa. Tunaona kila siku watu wazikwa,sijui wengine wanaamini wataishi Miele.....
 
View attachment 1625466
Jamaa aliniudhi sana na kuniangusha. Tumepiga kura wote kisha akanishawishi eti nitafute wenzangu kama 100 tupige kelele na kuandamana kama hatuna akili atanipa shillingi laki mbili., kumbe alishapanga tukio akamatwe aje kusingizia anataka kuuliwa ili akaishi Ulaya.Kwa kweli Lissu wewe ni msaliti, nataka hela zangu.
Mkuu acha urongo basi
 
Mkuu, Kama una uwezo wa kufanya chochote fuatilia mkoa wa Mara (hasa Tarime na Rorya), Simiyu na Singida. Utashangaa sana.

Pia, ukiacha Dar, naskia maeneo mengine mengi ni hivo hivo.

Wale unaskia wanakimbia usifikiri wanaigiza
Hapana. Mimi sisemi kuna kuigiza kwa wanaokimbia. Wanaokimbia wanajulikana na ni ushahidi usiopingika. Wanachokimbia kinajulikana na yeyote mwenye akili timamu isipokuwa hawa waliolewa waliomo humu JF na kwingineko.

Uzi huu ni muhimu sana. Unapoandika hapa kama ulivyoandika hata katika mistari mitatu uliyobandika hapo juu, huo sio ushahidi hata kidogo; hayo ni kama majungu tu.

"Mikoa ya Mara, Simiyu na Singida", wote hao hata mmoja tu asijulikane kabisa taarifa zake kwa usahihi?

Sasa usije ukadhani ninakukatalia kwamba watu hao hawapo, lakini kutaja tu mikoa bila hata ya taarifa zozote zinazowahusu watu hao, huo sio ushahidi. Hata hao wanaofanya maovu haya wanapenda sana taarifa za kijumlajumla sana kama hizi, kwa sababu haziwabani kivyovyote.

Watu wanaowekwa gerezani, kwa mamia, hata mmoja bila kutajwa jina na mkasa wake ukaelezwa na kueleweka..., huo sio ushahidi.
 
Kaka kule inbox umegoma kunipa mrejesho!
Utaniwia radhi ndugu yangu. Huko huwa napaepa kama ukoma; huwa siingii kamwe huko.
Naomba unielewe, na sio kwamba nakutilia mashaka mkuu wangu.

Tuendelee tu huku huku. Msimamo wako nauelewa barabara, na sina shaka nao.

Najua kuna siku moja tutaelezana yote bila ya shaka tunayoshindwa kuyaeleza bayana sasa hivi. Siku hiyo ipo tu inakuja.
 
Back
Top Bottom