Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

018056855f5b321a4e09839b7da4e486.jpg
 
Kupika kwanza
Keki nusu halaf vipimo sina itabidi ninunue,nishanunua hand mixer
Tafuta mzani
Na tin ya kupikia,sufuria huwa hazitoi keki yenye shape nzuri.


Recipe yule mdau Patra31 aliweka Jana.

Mixer siyo lazima uwe nayo.
Waweza tumia mwiko tu.
Hata mm sina mixer.


Sasa inabidi uandae moto
Kama ni oven inatakiwa uipashe iwe na moto
Au kama unatumia jiko la mkaa,
Unaandaa moto,unachukua sufuria kubwa sana unaweka mchanga kidogo,unaupika motoni.


Andaa tin yako mapema,unapaka siagi na unanyunyiza unga ili kuzuia keki kukakamia chini .


Unaanza sasa kuchanganya ingredients zako;
*Anza na siagi pamoja na sukari.
Hapa sasa ndipo pa muhimu..inatakiwa uchanganye kwa nguvu huu mchanganyiko hadi ugeuke kuwa na rangi nyeupe.

*Unaanza weka mayai
Unaweka moja baada ya jingine.
Kila ukiweka moja,unakoroga,unaongeza unakoroga
Hivyohivyo hadi unamlize.

*Anza kuweka unga wako
Hakikisha unga unauchekecha mapema.
Unaweka kidogo kidogoo.
Huu mchanganyiko wa unga usiupige sana kama ule wa siagi na sukari
Wenyewe tunachanganya tu kidogo..kama una mixer ,unaweka low speed.

Weka ladha matone kiasi tu.
Mimi huwa naongeza na vineger kijiko kimoja.

Kisha weka baking powder,koroga kiasi,

Usiache huu mchanganyiko ukae muda mrefu
Ukimaliza tu,unahamishia kwenye tin .
Igonge tin chini kama mara 3,kuondoa hewa hewa.
Usipogonga ndio zile keki unakuta Ina matobo.

Iweke tin ndani ya lile sufuria lenye mchanga wa moto .
Funika,weka moto juu.
Hakikisha moto hauwi mwingi sana wala mdogo sana.

Kama unatumia oven unaweka.

Usifunue funue keki Yako,inaweza kunywea.

Baada ya muda kama nusu saa hivi keki itakuwa tayari.
 
Back
Top Bottom