Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

IMG_8269.jpg
 
COOKIES/ BISCUITS
Ingredients.
1. Unga wa ngano vikombe 2
2. Sukari gram 200 / vijiko 13 vikubwa
3. Prestige/ siagi gram 200
4. Yai 1
5. Cornflower vijiko 2 vikubwa
6. Baking powder kijiko 1 kikubwa
7. Chumvi 1/4 kijiko.
8. Vanila 10ml

Uandaaji.
1.Weka sukari na pretige changanya mpaka ichanganyike vizuri iwe laini. Unaweza tumia machine au hata mkono. Ongeza yai na Vanilla uchanganye vizuri.

2.Changanya unga, baking powder na chumvi mpaka vichanganyike vizuri.

3. Chukua mchanganyiko wa unga, baking powder na chumvi uweke kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari.Kanda mpaka utakapokuwa tayari usiwe laini sana wala mgumu sana. Unaweza ongeza maziwa kiasi sio lazima.

4. Unaweza gawa mkando katika madonge kuweka ladha unayoitaka kama ni chocolate ( tumia cocoa powder), coffee nk.

5. Sukuma mkando wako na kata biscuits zako katika maumbo mbalimbali unayotaka wewe. Unaweza tumia shapes au machine maalumu. Kama huna kata kwa mkono tuu kutoa shapes.

6. Oka biscuits kwa moto wa wastanni 190 -200 c kwa dakika 10 zitakuwa tayari. Zitoe ziache zipoe na tayari kwa matumiziView attachment 2524786
Patra31
Naomba [emoji39][emoji39][emoji39]
 
Back
Top Bottom