Uzi wa vyakula tu

PopSawa hivi kwanin keki inapasuka??kwa juu
🎾MAKOSA UNAYOFANYA KATIKA UPISHI WA CAKE🎾

🎾CAKE KUWEKA MASHIMO SHIMO KWA NDANI
-Umetumia mayai mengi kuliko yanayotakiwa
-Hukuchanganya vizuri mchanganyiko wako wukawa sawa

🎾KEKI KUJAA MAFUTA
-Umetia siagi nyingi/mafuta mengi kuliko kipimo kinachotakiwa
-Umeyeyusha siagi, unatakiwa uitumie bila kuyeyusha
-Hukufuata vipimo

🎾CAKE INANATA KAMA INAUNYEVU
-Umetumia sukari nyingi
-umetiq mayai mengi
-umetumia unga mbaya tumia unga wa cake.
-umeacha sana kuitoa kwenye tin ikaweka unyevu
-maji mengi au maziwa

🎾KEKI HAIJAUMUKA
-Umetia baking powder kidogo/umeupiga sana mchanganyiko umeua nguvu ya bakingpoda
-Moto ulikuw mdogo
-chombo kilikua kipana sana
- umeacha sana mchanganyiko kabla hujaupika
-hukuchanganya mahitaji kama inavyotakiwa

🎾KEKI IMEWEKA MLIMA/ IMEPASUKA JUU
-Umeupiga sana mchanganyiko wa siagi au mayai
-moto ulikua mwingi

🎾KEKI IMEWEKA SHIMO KATIKATI
-Kufunua funua ukaingiza hewa.
-Moto mdogo
-sukari nyingi au siagi nyingi
-umechanganya sana mchanganyiko wako

🎾KEKI IMEKUA LAINI SABA MPAKA INAMOMONYOKA
-Umetumia sukari nyingi
-umetumiq baking poda nyingi
-umechanganya vibaya
umetumia mafuta/ siagi nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…