Uzi wa vyakula tu

Nataka nijipikilishehizi chapati za ndizi mzuzu na rosti ya kitimoto...πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹

Stay tuned, wacha nivute nguvu...

Mwanamke jiko, ukilivalia kaboka halikutupi...😜.

Your browser is not able to display this video.
 
Basi bwanaa....

Habari za akajasembamba zinafuata....





Rosti limekubali...πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹

Shughuli iko mtaa wa pili hapo eeheeee....

Hawakukosea waliosema iga ufe khaaa....

Hadi sturesi zikanipanda kisa msosi....πŸ₯²πŸ₯²

Ila nikakaza roho kula lazima ebooh πŸ˜›πŸ˜›


Hizo ndo zilikuwa malimbuko, yaani matoleo ya kwanza ya chapati za ndizi mzuzu eehehehehe jamanii....

Kujitia Kiranga tuu shughuli sii yangu hii khaa...!!

Sikukata tamaa, nikaongeza na zangu, nikapata chapati mfanano...


Hii ilikuwa chapati ya mwisho kupika, nilichanganya na unga wa ugali ili iweze kushikana kama chapati...πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹








Hizi nilichanganya na ngano ndo nikaweza unda hiyo chapati japo zimebabuka na moto ila akuuu, ni taamuuu...πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
 




Hapo tayari kulumangia, msosi wa kupika mwenyewe mtamu aiseeh sema tuu apetaiza ya kupika kila siku nehi...πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›



Shurbati ya beetroot carrots na apple...πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹



Niliongeza mara mbili ndo nikasema baassi tosha kwa leo.



Shiba kitumbo ndiii.....

Sasa wacha nikalime maana si kwa kushiba huku 😊😊😊.
 
Habari, naomba unitoe ushamba, hiyo picha ya kwanza hiyo kama nyama hua ni nyama mbichi? hua naona sana kwenye pictures, ni nyama ya nini na je ni mbichi kama inavyoonekana?
Hapana si mbichi hapo nimeshaikaanga

Ni bacon, ila hii ilikuwa bacon ya turkey (nafikiri ni bata mzinga).

Bacon πŸ₯“πŸ₯“ mara nyingi inakuwaga ya kitimoto ila hata za beef pia zipo.


View: https://youtube.com/shorts/VCykwtZLxSI?si=O4bRPjPY8iKg-50K
Elimu haina mwisho...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…