Mapishi ya kaimati.
Mahitaji:
Unga wa ngano vikombe viwili.
Mtindi wa cream bila flavour 75mls
Chumvi kdg tu.....like half a tea spoon.
Hamira one tea spoon.
Mafuta ya kupikia.
Maji kiasi.
Mahitaji ya shira :
Sukari vikombe viwili. Maji vikombe vitatu na nusu au vinne.
Iliki kijiko cha chai 1
Arki vanilla kiasi km kijiko cha chai lkn kisijae sana. Zafarani (saffron) ukipenda ziwe na colour kdg.
Unaanza na kutayarisha shira ili uiache ipoe. Changanya mchanganyiko wako wa sukari. Maji na Iliki. Arki unaweza kuweka hata mwisho ukiepua. Weka kwenye jiko kwa moto wa kiasi. Usiwe mkali sana. Iache ichemke mpk ianze kufanya vipovu kwa mbali (ikoroge kwa kijiko ili uangalie kama ishakuwa kiasi kama syrup mfano kama dawa za wtt iwe kama inanata kwa kuishika kwa vidole vya gumba na shahada)
Ikiwa hivyo epua halafu weka ile Arki yako na uiache ipoe.kadri ikipoa na ule uzito utazidi kdg.
Sasa unga wa kaimati. Changanya ingredients zako zote kasoro maji tu kwanza. Then anza kuweka maji kdg kdg huku unaupondaponda unga wako na kutoa vidonge vidonge vya unga. Fanya ivo mpk unga uwe smooth paste.
Mfano wake kama wa mikate ya ufuta au badia za unga wa dengu. Wengine huuchapa kwa mkono ili kuwa laini zaidi. Funika ili uumuke mara moja. Kiasi cha dkk 45 au lisaa (uangalie lkn maana Hamira nyengine zinaumua mara moja.
Unga wako ukisha umuka bandika karai jikoni. Weka mafuta ya kupikia kiasi kwa ajili ya deep frying. Mie nachota kwa mkono tu using my fingers. Kdg kdg mpk kiasi viingie vya kutosha kwenye karai. Koroga na mshebeki kugeuzageuza ili viive sawasawa vyote. Moto uwe kiasi tu. Moto mkali zitaungua na hazitaiva ndani. Hapa kunahitajika uvumilivu.
Zitapokuwa zimewiva kiasi zitoe zijigide mafuta kwenye chujio.
Rudia kuweka nyengine.
Wakati ushamaliza kuweka za round ya pili. Zile za mwanzo ziweke kwenye shira yako. Ziache zipate shira vizuri. Ukimaliza kuchoma za round ya pili zile za mwanzo zitoe kwenye shira weka kwenye bakuli lako la serving.
Rudia ivo ivo mpk umalize.
(Utopoweka kwenye shira unaweza kuzikorogea ili zishike vizuri shira.
Hope umenielewa. [emoji4][emoji108]
Picha umeziona? Zinaonesha kiasi zinavuotakiwa kuwiva. Picha ya tatu hapo ndio zipo kwenye shira. Na picha ya mwisho nishaziweka kwenye serving bowl.
All the best. And enjoy [emoji8]
View attachment 1767458View attachment 1767459View attachment 1767481View attachment 1767482