Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Sema dada ANGEL kwanini usiwe unaweka na somo la misosi, yaani namna ya kuandaa msosi flani. Mahitaji, matayarisho n.k

Unajua watu kama sisi ni food lovers, na tunapenda misosi amazing ya kibunifu na hiyo unayotupia humu.

Naomba uwe unatupa na somo namna ya kuandaa. Ikiwezekana anzisha hata group la mapishi huko whatsap. #CookWithAngel[emoji491][emoji490][emoji488][emoji1642][emoji1641][emoji487][emoji3053]
Ha ha haaaaa haaa. Noted mkuu
 
Haya basi usirudie mpnz
20210429_104127.jpg
 
nielekeze kupika kalmat
Mapishi ya kaimati.

Mahitaji:

Unga wa ngano vikombe viwili.
Mtindi wa cream bila flavour 75mls
Chumvi kdg tu.....like half a tea spoon.
Hamira one tea spoon.
Mafuta ya kupikia.
Maji kiasi.

Mahitaji ya shira :

Sukari vikombe viwili. Maji vikombe vitatu na nusu au vinne.
Iliki kijiko cha chai 1
Arki vanilla kiasi km kijiko cha chai lkn kisijae sana. Zafarani (saffron) ukipenda ziwe na colour kdg.

Unaanza na kutayarisha shira ili uiache ipoe. Changanya mchanganyiko wako wa sukari. Maji na Iliki. Arki unaweza kuweka hata mwisho ukiepua. Weka kwenye jiko kwa moto wa kiasi. Usiwe mkali sana. Iache ichemke mpk ianze kufanya vipovu kwa mbali (ikoroge kwa kijiko ili uangalie kama ishakuwa kiasi kama syrup mfano kama dawa za wtt iwe kama inanata kwa kuishika kwa vidole vya gumba na shahada)

Ikiwa hivyo epua halafu weka ile Arki yako na uiache ipoe.kadri ikipoa na ule uzito utazidi kdg.

Sasa unga wa kaimati. Changanya ingredients zako zote kasoro maji tu kwanza. Then anza kuweka maji kdg kdg huku unaupondaponda unga wako na kutoa vidonge vidonge vya unga. Fanya ivo mpk unga uwe smooth paste.
Mfano wake kama wa mikate ya ufuta au badia za unga wa dengu. Wengine huuchapa kwa mkono ili kuwa laini zaidi. Funika ili uumuke mara moja. Kiasi cha dkk 45 au lisaa (uangalie lkn maana Hamira nyengine zinaumua mara moja.

Unga wako ukisha umuka bandika karai jikoni. Weka mafuta ya kupikia kiasi kwa ajili ya deep frying. Mie nachota kwa mkono tu using my fingers. Kdg kdg mpk kiasi viingie vya kutosha kwenye karai. Koroga na mshebeki kugeuzageuza ili viive sawasawa vyote. Moto uwe kiasi tu. Moto mkali zitaungua na hazitaiva ndani. Hapa kunahitajika uvumilivu.
Zitapokuwa zimewiva kiasi zitoe zijigide mafuta kwenye chujio.

Rudia kuweka nyengine.
Wakati ushamaliza kuweka za round ya pili. Zile za mwanzo ziweke kwenye shira yako. Ziache zipate shira vizuri. Ukimaliza kuchoma za round ya pili zile za mwanzo zitoe kwenye shira weka kwenye bakuli lako la serving.

Rudia ivo ivo mpk umalize.

(Utopoweka kwenye shira unaweza kuzikorogea ili zishike vizuri shira.

Hope umenielewa. [emoji4][emoji108]

Picha umeziona? Zinaonesha kiasi zinavuotakiwa kuwiva. Picha ya tatu hapo ndio zipo kwenye shira. Na picha ya mwisho nishaziweka kwenye serving bowl.

All the best. And enjoy [emoji8]View attachment 1767458
20210426_162747.jpg
20210426_164716.jpg
20210426_171139.jpg
 
All the best. And enjoy [emoji8]View attachment 1767458View attachment 1767459View attachment 1767481View attachment 1767482
Haya ndiyo mambo sasa[emoji2956]
Ubarikiwe sana.

Ukipata muda tufundishe na mengine[emoji120]
 
we dada tafadhal tafadhali kama hujaolewa nakuomba PM. nahtaji kuwa na mwanamke anaejua na anaependa kupika kama hvyo. am serious asee.
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Braza vp ww si ushaoa bhanaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha mdogo ako nivute chombo hyo niaze kula mahanjumatt
 
Sijatoa talaka lakini na sitarajii kufanya hivyo asilani abadani[emoji3]
 
Back
Top Bottom