Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

1676372094761.png
 
Tafuta mzani
Na tin ya kupikia,sufuria huwa hazitoi keki yenye shape nzuri.


Recipe yule mdau Patra31 aliweka Jana.

Mixer siyo lazima uwe nayo.
Waweza tumia mwisho tu.
Hata mm sina mixer.


Sasa inabidi uandae moto
Kama ni oven inatakiwa uipashe iwe na moto
Au kama unatumia jiko la mkaa,
Unaandaa moto,unachukua sufuria kubwa sana unaweka mchanga kidogo,unaupika motoni.


Andaa tin yako mapema,unapaka siagi na unanyunyiza unga ili kuzuia keki kukakamia chini .


Unaanza sasa kuchanganya ingredients zako;
*Anza na siagi pamoja na sukari.
Hapa sasa ndipo pa muhimu..inatakiwa uchanganye kwa nguvu huu mchanganyiko hadi ugeuke kuwa na rangi nyeupe.

*Unaanza weka mayai
Unaweka moja baada ya jingine.
Kila ukiweka moja,unakoroga,unaongeza unakoroga
Hivyohivyo hadi unamlize.

*Anza kuweka unga wako
Hakikisha unga unauchekecha mapema.
Unaweka kidogo kidogoo.
Huu mchanganyiko wa unga usiupige sana kama ule wa siagi na sukari
Wenyewe tunachanganya tu kidogo..kama una mixer ,unaweka low speed.

Weka ladha matone kiasi tu.
Mimi huwa naongeza na vineger kijiko kimoja.

Kisha weka baking powder,koroga kiasi,

Usiache huu mchanganyiko ukae muda mrefu
Ukimaliza tu,unahamishia kwenye tin .
Igonge tin chini kama mara 3,kuondoa hewa hewa.
Usipogonga ndio zile keki unakuta Ina matobo.

Iweke tin ndani ya lile sufuria lenye mchanga wa moto .
Funika,weka moto juu.
Hakikisha moto hauwi mwingi sana wala mdogo sana.

Kama unatumia oven unaweka.

Usifunue funue keki Yako,inaweza kunywea.

Baada ya muda kama nusu saa hivi keki itakuwa tayari.
Umesahau kuniambia dakika ngapi kukoroga siag na sukar na mayai dakika ngapi
 
Nikinunua oven nataka ninunue kubwa itakayoweza kupika na zike cup cakes ndogo ndogo na nyingi .

Pia nitanunua nikishaanza rasmi biashara.

Sasahivi acha nikomae tu na mkaa.

Uzuri oven haina complications kama mkaa.
Nikiweza kwenye mkaa, hata Kwenye oven nitaweza.
Sema kwa biashara nunua oven ya gas au ya umeme na generator, vinginevyo utakuja pata hasara
 
Back
Top Bottom