Labda ni Ushamba zamani nilikuwa nahisi iPhone ndio kila kitu kwa upande wa smartphones nikapania kuimiliki mwaka juzi mwishoni nikafanikiwa kumiliki 8+ nikagundua kwasisi wa nchi maskini ni ngumu kuimiliki smartphone aina hii
1. Aichangamani na smartphone nyingine za Operating system tofauti na IOS.
2. App zake nzuri nyingi ni za kununua na ni kwa mfumo credit cards ambao sio common kwetu.
3. Wamiliki wake ktk mazingira yetu ni wachache hivyo ni vgm kupata watu wa ku share vitu
4.Kutokana na mazoea ya Android kuna kaugumu kwenye kuitumia na kukubaliana na mfumo wake.
5.App developer wengi hawaipi Umuhimu kwahiyo Apps nyingi hawazifanyiwi updates kulinganisha na App hizo hizo kwenye Android OS mfano rahisi ni hii "Jamii Forum" kwenye iPhone ina muonekano wa nyuma sana ambao kwenye Android ni version za longtime kitambo.
6.Inahitaji uwe njema mfuko hakuna cha bure ringtone lipia,Movies,Music nunua.
Ila general overview
1.Huwezi kuta zina stuck hovyo hovyo km simu za Android hasa Tecnos and alikes
2.App zake ni super hakuna yale ma App ya Android unayo download then unakuta haifanyi kazi husika "planks"
3.Hakuna mambo Ads kwenye iPhone tofauti na Androids yaani uko makini unatengeneza muamala Mara unashangaa limeingia tangazo "Dr Rajabu mtaalamu wa mitishamba"
4.Kwa upande wa Hardware niseme wako vzr hii simu yangu ninayo tu home toka ninunue haimjui fundi ,charger yake na cable sijawahi badili lkn hapa ndani nina mzigo wa USB cable na charger tofauti za simu za Android.
Sent using
Jamii Forums mobile app